Tuesday, October 11, 2022

Serukamba akemea wanaotumia mfumo wa makusanyo ya mapato kama kichaka cha kufichia maovu yao.

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ameitaka Halmashauri ya Itigi  wilayani Manyoni kuacha kusingizia  mfumo wa ukusanyaji wa mapato uitwao POS na  kuufanya kama kichaka cha kufujia fedha za Serikali.

Kauli hiyo ameitoa leo kwenye kikao chake na wakuu wa Idara pamoja na  wakusanya ushuru ambao hawakupeleka fedha hizo benki ambapo walieleza kwamba walishaleta fedha na kuzikabidhi Idara ya fedha lakini bado mifumo unasoma wanaodaiwa.

Kufuatia zoezi hilo RC Serukamba aliwahoji baadhi ya wakuu wa Idara ikiwemo Afisa Tehama kwamba inakuaje fedha zimelipwa lakini mfumo bado unaonesha mtu anadaiwa? ambapo Afisa Tehema alieleza kwamba mfumo huo huwa haupokei fedha nusu hivyo wanalazimika kufungua akaunti nyingine ambazo zinakusanywa fedha hizo mpaka zitimie kiasi kinachotakiwa.

Hata hivyo Serukamba alibainisha kwamba zaidi ya Milioni 248 hazijulikani zilipo kwa kuwa watoza ushuru wanaodaiwa wanakiri kupeleke fedha hizo Idara ya fedha  huku mifumo ikiwa haitambui kufanyika kwa malipo hayo.

Aidha Serukamba ametoa Siku Saba kwa watumishi walichukua fedha hizo kuzirejesha kabla ya kuchukuliwa hatua za Kisheria.

RC Serukamba ametoa wito kwa watumishi wanakusanya fedha hizo kuacha kukaa na fedha mikononi badala yake wazipeleke benki kwa kuwa huweza kuwaletea vishawishi na zikawaingiza matatani.


No comments:

Post a Comment