Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akitoa mchango wa fedha kwa ajili ya upasuaji wa macho kwa mgonjwa aliyekosa fedha kiasi cha shilingi elfu thelathini kwa ajili ya huduma za kibingwa Wilayani Mkalama.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata hududma za kibingwa katika hospitali ya Iambi ya Wilayani Mkalama.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dokta Rehema Nchimbi ameagiza Kliniki tembezi ya huduma za kibingwa kwa
mkoa wa Singida kuwa endelevu huku akizielekeza halmashauri kuandaa mpango wa
utekelezaji wa zoezi hilo kwakuwa linagusa maisha ya wananchi wa hali ya chini.
Amesema mara baada ya
kukamilika kwa halmshauri zote saba mpango wa kuanza kutoa huduma za kibingwa
kwa awamu ya pili uanze mara moja kwakuwa wagonjwa wengi walionufaika ni wale
webnye kipato duni na walikuwa wameshakata tama ya kupata matibabu.
Dokta Nchimbi
ametembelea wodi ya wanawake waliofanyiwa upasuaji na daktari bingwa wa
wanawake, wodi ya akina baba waliofanyiwa upasuaji wa magonjwa ya tezi dume na
matatizo ya njia ya mkopo pamoja, ametembelea chumba cha upasuaji wagonjwa wa
macho na kumalizia wodi ya watoto waliofanyiwa upasuaji kutokana na matatizo ya
mfumo wa upumuaji na midomo sungura.
Amesema, “Ukisikiliza
ushuhuda wa wagonjwa waliopatiwa matibabu ya kibingwa utaona umuhimu wa kliniki
tembezi, wengine walikwisha kata tamaa ya kuishi na kusubiria kifo, wengine
walitengwa na kusimangwa, kuna mmoja wakati analetwa hospitali kuonana na
madaktari hawa majirani waliwaambia ndugu zake watarudisha maiti lakini amepona
kabisa”.
Akitoa taarifa ya kliniki tembezi kwa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkalama Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta John Mwombeki amesema wagonjwa
walioonwa na madaktari bingwa kwa muda wa siku nne ni 675 na waliofanyiwa
upasuaji ni 71.
Dokta Mwombeki
ameeleza kuwa kliniki tembezi imekuwa na manufaa kutokana na kuwa na gharama
nafuu kuliko hospitali kubwa za rufaa ambapo wagonjwa wengi wameshindwa kufika
huko.
Naye Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Injinia Geofrey Sanga ameeleza kuwa halmashauri
yake imetoa milioni 18 kufanikisha zoezi hilo na kuahidi kuendelea kushikiana
na Mkoa katika awamu ya pili ili wananchi wote wenye uhitaji wa huduma za
madaktai bingwa wazipate.
Madaktari bingwa wa
magonjwa ya ndani, madaktari bingwa wanawake, wototo, macho, upasuaji, mifupa
na njia ya mkojo wametoa huduma za kibingwa wilayani Mkalama kuanzia Februari 27
hadi Machi 3.
Wakati huohuo Mkuu wa
Mkoa wa Singida amezindua rasmi kilimo cha korosho kwa kushiriki zoezi la upandaji
wa mikorosho na mihogo na kuhamasisha wananchi kupanda mikorosho hasa katika
mashamba yao waliyolima mihogo.
Dokta Nchimbi amesema
korosho ni zao linaloweza kuvunwa kwa zaidi ya miaka hamsini na pia ni rafiki
wa mazingira, huku akiendelea kusisitiza kilimo cha viazi lishe kwakuwa ni
mkombozi wa uchumi wa wananchi wa Singida.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akipanda Mkorosho katika shamba la Mkulima wa kijiji cha Gumanga wilayani Mkalama kama hamasa kwa wananchi wengine wapande zao hilo.
Wananchi wa kijiji cha Nkungi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wakisaidiana kupanda viazi lishe katika shamba la Mkulima ili kuhamasisha kilimo hicho.
No comments:
Post a Comment