Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kushoto) akizungumza na Karani wa Sensa (mwenye kishikwambi) wakati wa ziara wilayani Singida vijijini.
Serikali imetoa power benk 200 katika maeneo ambayo yanachangamoto ya ukosefu wa umeme Mkoani Singida kama sehemu ya utatuzi wa changamoto ya kuishiwa chaji kwa vishikwambi ambavyo vinatumiwa na Makarani wa Sensa ya watu na Makazi ya 2022.
Akiongea baada ya kuwatembelea
Makarani hao katika Manispaa ya Singida, Singida Dc na Wilaya ya Mkalama Mkuu
wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema Serikali imetoa Power Benk hizo kwa
kuwa jana uzoefu umeonesha baadhi ya maeneo Makarani kupata changamoto baada ya
vitendea kazi vyao kumaliza chaji kabla ya muda.
Amesema kutokana na ukaguzi alioufanya
kupitia Makarani wapata Tisa ameona zoezi linaendelea vizuri na kuna kila
dalili ya kumaliza zoezi hilo ndani ya muda na kila mwananchi kufikiwa.
RC Serukamba amawaomba wananchi wa
Mkoa huo kutoa ushirikiano mkubwa kwa Makarani ikiwemo kuwaruhusu kuchaji vishikwambi
vyao kwenye makazi yao wakati wakiendelea kuhesabu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Singida Mhandisi Paskas Muragili amesema zoezi linaendela vizuri na haijatokea
changamoto yoyote kwa kuwa wataalamu wa tehema wamekuwa karibu na Makarani kwa
ajili ya utatuzi wa changamoto yoyote itakayojitokeza.
Aidha amemhakikishia Mkuu wa Mkoa
kwamba kwa upande wa Wilaya ya Singida wanategemea mafanikio makubwa kama
walivyotegemea.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkalama
Sophia Kizigo ameeleza kwamba changamoto ya kuishiwa chaji imejitokeza kwa
Makarani wa Wilaya hiyo kwenye vijiji ambavyo havijapata huduma ya umeme.
Hata hivyo amemuomba Mkuu wa Mkoa
katika Power benk zilizokuja Wilaya hiyo ipewe kipaumbele kwa kuwa pamoja na
changamoto ya umeme kwa ajili ya kuchaji lakini bado kuna umbali wa nyumba hadi
nyumba.
Kizigo amewataka wananchi ambao
bado hawajahesabiwa kuhakikisha kuendelea kuwa na subira kwa kukuwa katika
kipindi cha siku Tano zilizobaki watahakikisha kila mwananchi anafikiwa.
Aidha Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Naing'oya Kipuyo amekiri kupokea power benk hizo ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwa Makarani waliyopangiwa Vijijini ambapo hakuna Umeme.
MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA ZIARA YA RC SERUKAMBA
Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Naing'oya Kipuyo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya ziara ya Mkuu wa Mkoa kukamilika.
No comments:
Post a Comment