Tuesday, August 09, 2022

RC Serukamba apokea Mwenge wa Uhuru, asema utakagua miradi yenye thamani ya Bilioni 8.2

 

Mwenge wa Uhuru Mkoani Singida umejipanga kukagua miradi yenye thamani ya Bilioni 8.28 ikiwa ni jumla ya miradi 35 inayohusu Elimu, Afya, Utawala bora, Maji, Barabara na uwezeshaji wa vijana kiuchumi.

Akihutubia leo tarehe 09.08.2022 Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba  baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Mseko kilichopo Wilaya ya Iramba  amesema kiasi hicho cha fedha kimejumisha Tsh.Milioni 84.203 ikiwa ni michango ya wananchi, Tsh.Milioni 173.29 ikiwa ni kutoka Halmashauri, Bilioni 6.449 kutoka Serikali Kuu na fedha kutoka kwa wahisani Sh.Bikioni 1.575.

Aidha amebainisha kwamba programu 18 zitazinduliwa na 11 zitawekewa jiwe la msingi ikiwa ni pamoja  na  programu 42 za Sensa, Rushwa, Malaria, Mapambano dhidi ya dawa za kulevya VVU na miradi ya Lishe.

RC Serukamba akaeleza kwamba katika kipindi cha awamu ya Sita Mkoa wa Singida umepokea jumla ya Tsh.Bilioni 270.371 kutoka Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na kwa wadau wengine kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Sekta ya Afya Utawala bora Kilimo Uwezeshaji wa vijana Sekta ya Barabara Nishati Maji na Habari na Mawasimiano.

Amesema sekta ya Afya jumla ya Sh.Bilioni 28.4 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali Nne (4), vituo vya Afya 15 na Ujenzi wa Zahanati utoaji wa chanjo na Ujenzi wa vyoo katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

Aidha RC Serukamba  amesema miradi mingine ni ya sekta ya Kilimo ambapo wakulima walipatiwa mbegu za ruzuku ya Serikali yenye thamani ya Tsh. Bilioni 2.26 zilizotolewa kwa wakulima wa Mkoa huo.

Hata hivyo amesema jumla ya vikundi 409 vya wanawake, vijana na wenye ulemavu vimefaidika na mfuko wa Taifa wa TASAF na kugharimu Tsh. Bilioni 12.07

Kwa upande wake Sahili Nyanzabara Geraruma Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa amezitaka kila Halmashauri kuhakikisha wanakuwa na nyaraka halisi zinazohusiana na miradi mbalimbali wakati wa ukaguzi.

Amesema kila Halmashauri inatakiwa kuonesha vielelezo vya namna ilivyo peleka fedha kwa vijana ikiwa ni pamoja na miradi iliyoanzishwa.

Amesema ni muhimu kuongeza usimamizi wa miradi ili iweze kuwasaidia wananchi kwa muda mrefu.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani, kimkoa yaliyofanyika katika kijiji cha Mseko wilaya ya Iramba mkoani Singida Agosti 9, 2022 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Sahili Nyanzabara Geraruma akipokelewa kwa gwaride kutoka vijana wa Skauti Mkoa wa Singida kwa lengo la kumvalisha skafu wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kimkoa yaliyofanyika katika kijiji cha Mseko wilaya ya Iramba mkoani Singida Agosti 9, 2022 





Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akiwapokea wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa yaliyofanyika katika kijiji cha Mseko wilaya ya Iramba mkoani Singida Agosti 9, 2022 


Shamrashara zikiendelea wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kimkoa yaliyofanyika katika kijiji cha Mseko wilaya ya Iramba mkoani Singida Agosti 9, 2022 



Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Sahili Nyanzabara Geraruma akipokelewa kwa gwaride kutoka vijana wa Skauti Mkoa wa Singida kwa lengo la kuvalishwa skafu wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kimkoa yaliyofanyika katika kijiji cha Mseko wilaya ya Iramba mkoani Singida Agosti 9, 2022 



Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru, wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kimkoa yaliyofanyika katika kijiji cha Mseko wilaya ya Iramba mkoani Singida Agosti 9, 2022 

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru, wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kimkoa yaliyofanyika katika kijiji cha Mseko wilaya ya Iramba mkoani Singida Agosti 9, 2022 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisoma taarifa ya miradi mbalimbali itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru, wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kimkoa yaliyofanyika katika kijiji cha Mseko wilaya ya Iramba mkoani Singida Agosti 9, 2022 


Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kushoto) akizungumza na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma mara baada ya mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kimkoa yaliyofanyika katika kijiji cha Mseko wilaya ya Iramba mkoani Singida Agosti 9, 2022 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Singida wakati wa hafla ya mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kimkoa.


Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Singida wakishiriki mapokezi ya Mbio hizo.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida pamoja na wasaidizi wake kutoka taasisi mbalimbali kwa kushiriki na mapokezi mazuri ya Mbio za Mwenge wa Uhuru yaliyofanyika katika kijiji cha Mseko wilaya ya Iramba mkoani Singida Agosti 9, 2022 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda mara baada ya mapokezi ya kimkoa yaliyofanyika katika kijiji cha Mseko wilaya ya Iramba mkoani Singida Agosti 9, 2022 

KAULI MBIU:
SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO
SHIRIKI KUHESABIWA, TUYAFIKIE MAENDELEO YA TAIFA
www.singida.go.tz

No comments:

Post a Comment