Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Agosti 10, 2022
Akiongea wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru huo
kutoka Wilaya ya Iramba, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo amesema kwamba Mwenge
utakagua miradi ya Ujenzi wa shule kupitia fedha za Uviko Vituo vya Afya na Miradi
ya Lishe.
DC Kizigo amebainisha kwamba mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zitakagua
miradi hiyo ambayo imegharimu jumla ya Tsh. Bilioni 1.34 na kwamba utawasaidia
wananchi wengi wa Wilaya hiyo.
Awali akikabidhi Mwenge wa Uhuru, DC Suleiman Mwenda aliwakumbusha
wana Mkalama kujipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kuandaa nyaraka halisi za
miradi hiyo.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge Sahili Nyanzabara Gerurama ameanza kwa kutoa neno la Sensa ambapo
amewataka wananchi kujitokeza kuhesabiwa
tarehe 23.8.2022 katika kukamilisha zoezi la Sensa ya watu na makazi.
Aidha amewataka viongozi katika Halmashauri hiyo pamoja na
Wahandisi husika kuhakikisha katika eneo la Mradi kunakuwepo na nyaraka
zinazotakiwa na watu watakaoweza kutoa maelezo sahihi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment