Waziri Mkuu Kasim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Takukuru
Mkoa wa Singida kuwachunguza wakusanyaji wa mapato Wilayani Manyoni kwa kuhusika na upotevu wa mapato
katika standi ya mabasi Wilayani hapo.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo kwenye ukumbi wa mikutano
wa RC Mission Itigi alipokutana na Watumishi wa Halmashauri ya Itigi na Manyoni
ambapo alibainisha kwamba kuna upotevu mkubwa wa mapato katika stendi ya mabasi
kunakotokana na matumizi yasikuwa sahihi ya posi.
Amesema jumla ya mabasi yanayoingia kwenye stendi ya mabasi
ni zaidi ya 200 kwa Siku na kila Basi linatozwa Tsh. 2500 lakini bado
Halmashauri hiyo imekuwa ikikusanya TSH. Milioni moja na laki Saba (1,700,000)
kwa mwezi huku akifafanua kwamba kutokana na uchunguzi uliofanyika hivi
karibuni ulibainisha bàadhi fedha kutopelekwa Benki jambo ambalo linazua
sintofahamu juu yake.
Waziri Mkuu ameeleza kwamba baada ya Serikali kuona upotevu
wa mapato hayo waliweka mtu mwingine ambaye katika kipindi cha wiki mbili
alieleza kukusanya kiasi cha Milioni zaidi ya 20 hivyo kumtaka Kamanda wa Takukuru
kuchunguza upotevu huo.
Aidha amewataka Maafisa wote ambao wanahusika katika zoezi la
ukusanyaji wa mapato kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU ili kuhakikisha waliohusika
wanapatikana na fedha zinajulikana
zilipokwenda.
Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wote wa Halmashauri
hizo kuhakikisha wanasimamia miradi iliyopo ili iweze kuwanufaisha wananchi.
No comments:
Post a Comment