Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo Wilayani hapo baada ya kupata malalamiko ya
wananchi wa maeneo hayo wakilalamikia kushindwa kukamilika kwa Barabara hiyo
kwa kipindi kirefu na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo.
Aidha Waziri Mkuu akamuagiza Meneja TARURA Mkoa wa Singida
kukagua na kumlipa Mkandarasi kulingana na asilimia zilizofikiwa katika Ujenzi
wa Barabara hiyo na asilimia zilizobaki apatiwe Makandarasi mwingine
atakayeweza kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
Hata hivyo kutokana na kutokamilika kwa miradi mbalimbali
Wilayani Manyoni ikiwemo Mpango wa wamachinga, Ujenzi wa masoko kutokutana na
wananchi kusikiliza changamoto zao Waziri Mkuu akawahakikishi wananchi kwamba
viongozi wote ambao walihusika katika kukwamisha miradi ya Serikali
kutokamilika watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Malalamiko mengine ya
wananchi hao ilikuwa ni kutozwa fedha wakati wa kujifungua kina mama
wajawazito ukosefu wa masoko huduma isiyoridhisha wa stand ya mabasi na madeni
ya fidia ya ardhi ya wananchi.
Aidha Waziri Mkuu akawaahidi wananchi hao kushughulikia swala
la madeni ya fidia za ardhi pamoja na changamoto ya Kodi huku akimtaka mkuu wa
Mkoa kuhakikisha wanakuja kuwasikiliza wafanyabiashara wadogo maarufu Kama
wamachinga ili kutatua changamoto zilizopo.
Matukio katika picha
No comments:
Post a Comment