Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Binilith Mahenge ametembelea miradi ya maendeleo ikiwemo ya Afya shule na miradi ya maji iliyopo halmashauri ya Itigi na wilaya ya Ikungi ili kujionea mipango na mikakati ya kumaliza miradi hiyo kwa wakati.
Akiwa katika ziara hiyo Mahenge amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha ubora unazingatiwa katika miradi hiyo pamoja na kuzingatia sheria na taratibu za manunuzi ili kuhakikisha kwamba thamini ya fedha inakuwepo.
Amesema zoezi la ukaguzi wa miradi mbalimbali Mkoani hapo litakuwa endelevu na atakuja bila kutoa taarifa lengo likiwa ni kupata miradi ile iliyokusudiwa.
Miradi iliyotembelewa ni Kituo cha Afya Mitundu kilichogharimu Milioni 250 ambazo zinatakiwa kujenga majengo zaidi ya matatu
Mradi mwingine ni Mradi wa Kisima ambao upo katika Kijiji cha Guhungu kata ya Sanjaranda Halmashauri ya Itigi na unagharimu kiasi cha Milioni 226 mpaka kukamilika utakamilika tarehe 30 .8.2022
Aidha Mradi mwingine ni Ujenzi wa shule mpya eneo la Kitaraka Itigi ambapo zaidi ya Milioni 470 zitatumika kujenga majengo Saba ya Utawala madarasa nane na ofisi, Maktaba, vyumba vitatu vya Maabara, matundu 17 ya vyoo pamoja na ujenzi wa Tanki la maji.
Miradi mingine ujenzi wa vyumba vya madarasa na mradi wa maji na nyumba za wafanyakazi katika Wilaya ya ikungi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment