Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa Majaliwa akizungumza na wananchi katika Kituo cha Afya Mtoa mara baada ya kuweka jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Mtoa wilayani Iramba.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo akiwa katika muendelezo wa
ziara yake katika Kata ya Mtoa Wilayani
hapo wakati wa kuweka jiwe la msingi
katika kituo cha Afya cha Mtoa kilicho
gharimu Tsh. Milioni 662
Amesema kwa jographia
ya Wilaya ya Iramba vijiji vipo mbali na
ofisi za Serikali jambo ambalo inawagharimu fedha nyingi kufika kwenye ofisi
hizo kupata huduma.
"Leo mimi nimetoka ofsini kwangu nimekuja Kata ya Mtoa
kutatua kero za Wananchi sasa na nyie watumishi wa umma mtoke ofsini
mkawahudumie wananchi huko walipo" Alisema
Aidha amewataka watumishi kuwa waaminifu na kusimamia maadili
ya utumishi wa umma ili kutumia utaalamu wao kuleta matokeo chanya.
Amesema watumishi wahakikishe wanawasikiliza wananchi na
wasiwafukuze maofisini badala yake waende Vijijini kuwaeleza fursa ambazo
zinatekelezwa na Idara mbalimbali kama Afya na kilimo.
"Shirikianeni na Madiwani kuwafikia wananchi na
waelezeeni mafanikio ya Serikali, nendeni kwa wananchi mkawape huduma na
kusikiza kero zao".
Waziri Mkuu akaendelea kusema kwamba kumekuwepo na changamoto
ya usimamizi wa vyanzo vya mapato hivyo
kusababisha upotevu na hasara kwa Serikali hivyo kuwataka wakuu wa Idara
kutekeleza majukumu yao na kila Idara ihakikishe inafanya kazi yake ili kuleta
mabadiliko.
Waziri Mkuu amewataka Maafisa Tawala wa Wilaya kuhakikisha
kwamba watumishi wanatekeleza majukumu yao na wanakuwa na maadili ndani ya Halmashauri
na kuwachukulia hatua wote watakaokwenda kinyume.
Katika hatua nyingine ameeleza kuhusu utunzaji wa mazingira
na vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kulinda miradi ya maji ambayo Serikali
imetumia fedha nyingi kuitengeneza.
Waziri Mkuu amezitaka kamati za maji na Mazingira kusimamia
vyanzo vya maji na kuzuia uharibifu wa
Mazingira ili kuongeza upatikanaji wa maji kama ilivyokuwa awali.
Aidha amesema awali maji yalikuwa yakitiririka maeneo mengi
katika Kata hiyo lakini kwa sababu mifugo imekuwa ikiingizwa katika vyanzo vya
maji na kwenye hifadhi za mazingira.
Amesema Misigiri imekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji
kwa muda mrefu lakini changamoto hiyo
itakwisha kwa kuwa mradi wa maji
umekamilika hivyo kila nyumba utapata maji alisisitiza Waziri Mkuu.
Katika mwaka wa fedha wa 2021/22 Serikali imetenga Bilioni
5.1 kwa aji ya miradi ya maji katika Wilaya ya Iramba ikiwa ni pamoja na mradi
wa maji kutoka Ziwa Victoria aliendelea kueleza Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment