Tuesday, October 05, 2021

Msimu wa kilimo 2021/22 waanza hivi karibuni, Wakulima watakiwa kujiandaa


Wakulima Mkoani Singida wametakiwa kujiandaa na msimu wa kilimo wa mwaka 2021/22 unaoanza hivi karibuni kwa kukutanishwa na Wadau wa pembejeo za kilimo.

Beatusi Choaji, Katibu Tawala Msaidizi uchumi na uzalishaji amebainisha hayo leo alipotembelewa na waandishi wetu ofisini kwake Mkoani hapa.

Amesema Mkoa tayari wameshaanza uzinduzi wa msimu wa kilimo katika halmashauri ya Singida DC, Mkalama pamoja Iramba ambapo lengo ni kufanya katika halmashauri zote saba ili kuwakutanisha wakulima pamoja na wauza pembejeo za kilimo.

Bw. Choaji amesema wakulima kupitia makampuni mbalimbali ya pembejeo watakopeshwa mbegu na pembejeo nyingine kama walivyofanya mwaka jana ambapo malipo yatafanyika baada ya wakulima kuvuna.

 Amebainisha kwamba katika kikoa chao cha hivi karibu kilichohusisha makampuni ya kuuza pembejeo za kilimo Agro dealers  tayari makampuni zaidi ya matatu yalijitokeza lengo likiwa ni  kushirikiana na vyama vya msingi AMCOS katika kupata  njia rahisi ya usambazaji wa pembejeo hizo.

No comments:

Post a Comment