Watanzania wametakiwa kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa zoezi la Sensa ya majaribio kwa mwaka 2021 ya watu na makazi litakalofanyika katika vijiji 13 vya Tanzania bara katika mikoa ya Kigoma, Singida, Arusha, Dar es salaam, Mwanza, Morogoro, Mtwara, Njombe na Dodoma.
Akizungumza na
wananchi hivi karibuni katika kitongoji cha kijaroda wilaya ya Mkalama mkoani
Singida Kamisaa wa Sensa ambaye pia ni spika
mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna
Semamba Makinda amesema sense hiyo ya
majaribio itaanza tarehe 08 mpaka 19 mwezi huu hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kufanikisha zoezi hilo.
Aidha amesema zoezi la sensa ya majaribio kwa mwaka 2021
litatoa mwelekeo, fursa na changamoto katika
kujipanga na sensa ya mwaka 2022.
“Tukifanya vizuri mwaka huu
itakuwa ni dalili ya kufanya vizuri Zaidi mwaka kesho kwa sababu
tutakuwa tumejifunza kutokana na
changamoto za kipindi hiki” alisema Makinda.
Amesema sensa ya mwaka huu itakuwa ni tofauti na vipindi
vingine ambayo ilikuwa inaishia katika ngazi ya wilaya na mkoa lakini kwa mwaka
huu na mwaka kesho itakuwainafanyika hadi ngazi ya kitongoji.
Lengo la sensa hii ni kutaka kufahamu juu ya makazi majengo, anuani,
idadi ya watoto, vijana na wazee ambao wapo ili waweze kuendana na bajeti ya Serikali.
Alibainisha mama Makinda.
Aidha mama Makinda amesema sensa ni muhimu kwa taifa kwa sababu itasaidia kusukuma gurudumu la maendeo ya jamii, kusaidia kuratibu uwepo wa miundombinu ya shule, hospitali, barabara, makazi na hata mikopo kwa wanafunzi.
Akimalizia hotuba yake Kamisaa wa sensa Mama Makinda amewatoa
hofu wananchi kwamba makarani watakaohusika katika zoezi hilo wamepata mafunzo
ya kutosha na wamekula kiapo cha kutunza siri za watu wakati wa kuhesabu.
Naye mratibu wa sensa katika ngazi ya mkoa wa Singida Bw. Naeng’oya
Kipuyo amesema maandalizi ya sense mkoani hapo yamekamilika kwa kuwa tayari
maeneo yameshatengwa na uhamasishaji umefanyika kwa kiasi kikubwa.
Amebainisha kwamba sensa ya majariibio kwa mkoa wa Singida itafanyika
kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe nane (8)
mpaka 10 ambapo wataalamu watangazia
huduma za kijamii zinazopatikana eneo
hilo.
Usiku wa tarehe 10 kumkia tarehe 11 itafanyika sensa ya majaribio
katika Kitogoji hicho kuhesabu watu waliolala katika nyumba zao zoezi
litakalochukua siku tatu (3) mpaka tarehe 13 alibainisha bwana Kipuyo.
Amesema tarehe 14 mpaka 16 zoezi la sensa litaendelea katika Kitogoji
hichio cha Kijaroda ambapo itafanyika sensa ya majengo, wamiliki na huduma
zinazofanyika katika nyumba hizo na mwisho ilatakuwa ni kuchukua anuani za makazi kwenye kila
nyumba alimalizia bwana Kipuyo.
Mery christiani ni msichana mkazi wa Kitogoji hicho
ameishukuru Serikali kwa hatua hiyo na kuwasihi wananchi kutokuwa waoga na
kuhakikisha wanajitokeza kuhesabiwa ikiwa ni
pamoja na wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata mahitaji yao ya baadae.
Matukio katika picha
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Mfaume Kizigo (kushoto) akihutubia wananchi kuhusu umuhimu wa sensa ya watu na makazi katika eneo hilo.
Afisa uhamasishaji wa sensa Bw. Andrew Punjila akiwagawia wananchi vipeperushi vya elimu ya sensa na umuhimu wake wakati wa mkutano huo.
Mkutano ukiendele katika Kitongoji cha Kijaroda
No comments:
Post a Comment