Dkt. Nchimbi amesema fulsa nyingine katika maonesho haya ni wajasiriamali kukutana kwa pamoja na kunufaika na fulsa kubwa ambazo zinatengenezwa na maonesho haya ikiwemo fulsa ya masoko.
“Hapa tutaone teknolojia
mbalimbali ambazo zinauwezo mdogo, wa kati na zenye uwezo mkubwa. Tutakutana pia
na milango ambayo tulifikiri haipo kumbe ipo kwa ajili ya bidhaa mbalimbali
tunazozizalisha kwa kutumia malighafi zetu katika viwanda vyetu” Dkt. Nchimbi
Kwaupande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Bw. Silvester Mpanduji amesema
maonesho haya yanatarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani ya
Tanzania na nchi zaidi ya 6 ili kuonesha teknolojia mbalimbali zinazotumika katika kutengeneza bidhaa mbalimbali kupitia viwanda
vidogo, vya kati na vikubwa.
Akifafanua zaidi amesema kutakuwa
na wajasiriamali kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Afrika Kusini, Namibia, Kenya, India na
China ambapo teknolojia mbalimbali mahususi zitaoneshwa ambazo watu wakiziona watashawishika
kwenda kuzitumia na kuanzisha viwanda.
Aidha, ametoa wito kwa watanzania
kwenda kutembelea ili kuona na kununua bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu
na kusisitiza kuwa sasa ni wakati muafaka kwa Watanzania kutumia bidhaa
zinazozalishwa hapa nchini kwani ni bora na zenye viwango vya juu.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa masoko
na uwekezeji mkoa wa Singida Bi. Shoma Kibende amesema huduma zote za SIDO
zitakuwepo wakati wa maonesho ikiwemo ushauri wa kiteknolojia na jinsi ya
uanzishaji viwanda na uboreshaji, mafunzo ya kibiashara na
ufungashaji ulio bora na utumiaji wa vifungashio.
Pia kutakuwa na siku ya kuenzi au kuhamasisha utumiaji wa bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani ya Tanzania pamoja na uhamasishaji wa mazao mbalimbali yakiwemo alizeti, korosho na mazao mengine.
Amesisitiza kuwa katika maonesho
haya taasisi mbalimbali zitakuwepo ili kutoa huduma ikiwepo Taasisi ya usajili (BRELA) na Taasisi ya Uongezaji Ubora (TBS).
“NDUGU
ZANGU NINAWAKARIBISHA NA NINAAMINI HAKUNA MTU ATAKAYEKOSA MAONESHO HAYA
MAKUBWA”
DKT. NCHIMBI
Imetolewa na;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
SINGIDA
No comments:
Post a Comment