Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa, Balozi Dk. Augustine Mahiga (MB), akimkabidhi mtoto wa umri chini ya miaka mitano cheti cha kuzaliwa, wakati wa uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano. Uzinduzi ulihusisha mkoa wa Singida na Dodoma, umefanyika mkoani Singida.
SERIKALI imewataka viongozi na wananchi kwa ujumla kutambua kuwa
mfumo thabiti wa usajili na vifo ni kichocheo cha ukuaji kwa sekta ya viwanda
nchini, hivyo wana wajibu kushiriki kikamilifu kampeni inayoendelea ya kusajili
watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Wito
huo umetolewa (21/03/2019) na Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa, Dk. Augustine
Mahiga (MB), wakati akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi wa mpango wa
kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano. Uzinduzi
huo uliohusu mkoa wa Singida na Dodoma, umefanyika katika kituo cha zamani cha
mabasi ya mikoani mjini Singida.
Mheshimiwa,
Dk. Augustine Mahiga (MB), amesema kuwa mwekezaji akitaka kujenga kiwanda cha
bidhaa za watoto mkoani Singida, ni lazima apate takwimu sahihi za watoto walipo
katika mkoa huu, na pia mikoa jirani. Pengine hata akahitaji takwimu za watoto
nchi nzima.
Amesema,
mwekezaji anaweza kuhitaji kujua kiwango cha ukuaji wa idadi ya watu
(‘population growth rate’). Sababu kubwa ikiwa ni kupata uhakika wa soko la
bidhaa zake kwa miaka ijayo.
“Mpango
tunaouzindua leo (21/03/2019), una majawabu ya mahitaji yote niliyoyataja, hivyo
kuanzia leo viongozi na wananchi sote tutambue umuhimu wa kusajili
watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano” Dk. Mahiga.
Akisisitiza, Dk. Mahiga amesema, Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimabli kwa
lengo la kuleta maboresho ya mfumo wa usajili kupitia mkakati wa kitaifa wa
usajili matukio muhimu ya binadamu na takwimu.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa, Balozi Dk. Augustine Mahiga (MB), akizungumza na wananchi, wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano. Uzinduzi huo umehusisha mkoa wa Singida na Dodoma, umefanyika mkoani Singida.
“Kitendo hiki ni maamuzi ya Serikali ya awamu ya TANO, natuhinishe
kitendo cha uandikishaji na muono wa Rais wetu Mheshimiwa Dk. John Pombe
Magufuli. Uandikishaji ulikuwepo lakini umepewa umuhimu na kiongozi ambaye
anamaono makubwa kuhusu watoto na maendeleo yao. Na unaposema mtoto unasema
mama. Maendeleo hayaji bila takwimu”.
“RITA
ikiwa kama moja ya taasisi katika wizara yangu, tunafanya kazi kwa karibu pamoja
na wadau wengine, kuhakikisha kwamba mkakati huu wa usajili unakubalika na
kueleweka kwa wadau mbalimbali ili kuweza kuingizwa katika mipango ya nchi”, Dk.
Mahiga.
Aidha,
Dk. Mahiga amesema ataendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya mpango wa
usajili wa watoto huku akisisitiza kuwa utamaduni wake ni kufuatilia jambo kwa
karibu na hapendi kuzindua kitu ambacho hakitafanikiwa.
Awali,
Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu, Bi. Emmy K. Hudson, amesema huduma za usajili wa
watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano sasa umesongezwa karibu
zaidi kwa wananchi. Sasa utafanyikia kwenye ofisi za watendaji wa
kata na vituo vya afya vinavyotoa huduma za afya za mama na mtoto.
Kwa
mujibu wa Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu Bi. Emmy, amesema utekelezaji wa
kampeni hii katika mikoa ya Singida na Dodoma awamu ya kwanza hadi sasa zaidi
ya watoto 2,987,629, wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.
Kupitia
mpango huu, wastani wa kitaifa umepandishwa kwa zaidi ya asilimia 15
awamu ya kwanza na kufikia zaidi ya asilimia 38.5. Tunategemea takwimu hizi
kubadilika muda mfupi ujao baada ya kumaliza bakaa la watoto wasio na vyeti vya
kuzaliwa katika mikoa ya Dodoma na Singida ambao ni zaidi ya watoto 665,060.
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umefanikiwa kusajili
Watoto Milioni tatu na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa bila ya malipo kupitia
Mpango wa usajili wa Watoto walio na umri chini ya miaka mitano unaoendelea
kutekelezwa katika Mikoa kumi na mitatu Tanzania Bara.
MUHIMU:
(Cheti hiki kinatolewa bila malipo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, cheti cha kuzaliwa sio uthibitisho wa Uraia).
MATUKIO KATIKA PICHA
Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa, Dk. Augustine Mahiga (MB), akisalimiana na Mheshimiwa Meya wa Manispaa ya Singida Alhaji Mbua Chima mara baada ya kuwasili katika eneo la tukio la sherehe za uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano. Uzinduzi huo umehusisha mkoa wa Singida na Dodoma, umefanyika mkoani Singida.
SEHEMU YA MEZA KUU
Kikundi cha Mbalamwezi kutoka Manispaa ya Singida kikiburudisha wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano. Uzinduzi huo umehusisha mkoa wa Singida na Dodoma, umefanyika mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mheshimiwa Mhandisi Pascas Muragili akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano. Uzinduzi huo umehusisha mkoa wa Singida na Dodoma, umefanyika mkoani Singida.
Kaimu, Kabidhi Wasii Mkuu, Bi. Emmy Hudson, akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano. Uzinduzi huo umehusisha mkoa wa Singida na Dodoma, umefanyika mkoani Singida.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju, akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano. Uzinduzi huo umehusisha mkoa wa Singida na Dodoma, umefanyika mkoani Singida.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa, Balozi Dk. Augustine Mahiga (MB), akifurahia jambo wakati Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju alipokuwa akizungumza na wananchi katika sherehe za uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano. Uzinduzi huo umehusisha mkoa wa Singida na Dodoma, umefanyika mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi akizungumza na wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano. Uzinduzi huo umehusisha mkoa wa Singida na Dodoma, umefanyika mkoani Singida.
Shamla shamla za hapa na pale zikiendelea wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano. Uzinduzi huo umehusisha mkoa wa Singida na Dodoma, umefanyika mkoani Singida.
IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA
SINGIDA
No comments:
Post a Comment