Friday, December 21, 2018

RC SINGIDA, DKT. REHEMA NCHIMBI AONGOZA KIKAO CHA WADAU WA MAPATO YA SERIKALI ILI KUONGEZA WIGO WA KODI


Mkuu wa mkoa wa SINGIDA Dkt. REHEMA NCHIMBI amewaagiza watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa SINGIDA kutumia lugha rafiki pindi wanapoenda kudai kodi kwa wafanyabiashara kwani kwa kufanya hivyo kutawatia moyo wafanyabishara hao kulipa kodi kwa hiari bila kulazimishwa.

Mkuu huyo wa mkoa wa Singida ameyasema hayo katika mkutano na wadau mbalimbali wa kodi mkoani hapa, uliyolenga kujadili namna ya kutanua wigo na kuongeza mapato ya Serikali.

Dkt. Nchimbi amesema watendaji hao wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kuelimisha wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo umuhimu wa kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Naye, Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt. ANGELINA LUTAMBI amesema mapato yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Singida hayalingani na fedha ambazo zinatengwa Serikali kuu kwa ajili ya shughuli za maendeleo mkoani hapa hivyo ni muhimu kwa wafanyabishara waongeza ulipaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Aidha, katika hatua nyingine, Dkt. Nchimbi aliwapatia Wakuu wa Wilaya husika vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo wenye sifa elekezi waliopo katika kila wilaya ndani ya mkoa wa Singida.

Kwa sasa mkoa wa Singida unajumla ya walipa kodi elfu 16,732 walioandikishwa lakini walipakodi walio hai ni elfu TISA na 550 Tu.

 Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. ANGELINA LUTAMBI akizungumza na wadau mbalimbali wa kodi katika kikao cha kujadili namna ya kutanua wigo na kuongeza mapato ya Serikali, kilichofanya katika ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

 Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Singida Bw. Apili Mbaruku akizungumza na wadau mbalimbali wa kodi katika kikao cha kujadili namna ya kutanua wigo na kuongeza mapato ya Serikali. 

 Viongozi wa DINI mbalimbali mkoa wa Singida wakifuatilia kikao kwa makini namna ya kutanua wigo na kuongeza mapato ya Serikali. 



Wadau kutoka sekta mbalimbali mkoani Singida wakizungumza katika kikao cha kujadili namna ya kutanua wigo na kuongeza mapato ya Serikali,  kilichofanya katika ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

 KATIKA HATUA NYINGINE


  Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskasi Muragili akipokea vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo wenye sifa elekezi waliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Singida mkoani Singida.  



 Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanueli Luhahula akipokea vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo wenye sifa elekezi waliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida. 

 Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka akipokea vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo wenye sifa elekezi waliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.



 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu akipokea vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo wenye sifa elekezi waliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.


Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Rahabu Mwangisa Solomon akipokea vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo wenye sifa elekezi waliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Manyoni  mkoani Singida.



IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO, 
OFISI YA MKUU WA MKOA, 
SINGIDA

No comments:

Post a Comment