Mkuu wa Mkoa
wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewahimiza Watanzania kununua na kutumia bidhaa
zinazotengenezwa na Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) nchini ili kukuza uchumi na
kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania.
Mkuu wa
mkoa wa SINGIDA ametoa wito huo katika Mahafali ya wanafunzi wa Chuo cha Ufundi
Stadi RC Mission VTC wilayani Manyoni mkoani Singida alipokuwa akizungumza na
wahitimu, wanafunzi, wazazi na viongozi mbalimbali wa Serikali ya halmashauri
ya wilaya ya Manyoni waliohudhulia Mahafali hayo.
Dkt. Nchimbi katika mahafali hayo amesisitiza, Halmashauri zinapaswa kutambua
maarifa na matunda ya vyuo vya ufundi stadi VETA kwa kutangaza bidhaa zao kwani zinatengenezwa kwa
ufanisi na ubora unaotakiwa.
Mahafali
ya wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi RC Mission VTC, Wilayani Manyoni mkoani
Singida, yaliambatana na maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanafunzi
hao ikiwemo fanicha, nguo mbalimbali (batiki), pamoja na huduma za magari na umeme.
Kwa upande wao wahitimu wa chuo cha ufundi stadi RC Mission VTC wameiomba Serikali ya halmashauri ya Manyoni kuwatambua wanafunzi hao kwa kazi nzuri wanazofanya.
Jumla ya
wanafunzi 49 wamehitimu mafunzo ya Ufundi Stadi kati ya hao wasichana waliohitimu ni 4, suala ambalo
Dktr. Rehema Nchimbi amesema wasichana wanapaswa kutambua nao wanahaki sawa
kama ilivyo kwa wanaume, na kuahidi kuwalipia ada wanafunzi wa kike 3 kwa fani
ya umeme 1 na ufundi magari 2, ikiwa kama motisha kwa wengine.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA
SINGIDA
No comments:
Post a Comment