Monday, November 05, 2018

MKOA WA SINGIDA WAWEKA MIKAKATI YA KUONGEZA UZALISHAJI WA ZAO LA ALIZETI KWA MWAKA 2018/2019


Serikali ya Mkoa wa Singida imeanza kuchua hatua katika kuhakikisha inaongeza maradufu uzalishaji wa zao la Alizeti ambalo ni zao mkakati la Mkoa huo kwa kuhakikisha upatikanaji wa mbegu bora katika msimu wa kilimo wa 2018/2019 ambazo zitasambazwa kwa Wakulima.

Akifungua mkutano wa Mkakati wa Upatikanaji wa Mbegu Bora za Alizeti kwa Msimu wa 2018/2019, Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema moja ya mkakati wa Mkoa ni kuhakikisha Wakulima wote wa Alizeti wanapata Mbegu Bora na kwa wakati na kuondoa matumizi ya mbegu hasara.

"Mkoa wa Singida kufuatana na hali ya hewa na kiasi cha mvua inachopata na aina ya udogo wake zao kuu na ambalo limeibeba Singida na linaihakikishia kuibeba Singida kwa mabadiriko makubwa sana ya kiuchumi na maendeleo ya wananchi wake ni zao la Alizeti"

"Mkoa wa Singida umelima Alizeti kwa miaka mingi na ninawashukuru sana wananchi na ninawapongeza kwa namna ambavyo wamelipokea hili zao la Alizeti na wamekuwa wakilima na tunaona mabadiriko makubwa ya maisha ya Wananchi"

"Leo tumeona tukutane na wadau wote wanaohusika na kilimo cha alizeti ili tuweze kufanikiwa katika kufanikisha kilimo cha alizeti kinafikia malengo na makusudi na matazamio ya Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba tuweze kuzalisha mafuta ya kutosha ya chakula ili kupunguza kile kiwango cha kuagiza mafuta kutoka nje, ni lazima sisi wakulima wa Alizeti kutoka mkoa wa Singida na wadau wote tuwe pamoja"

"Mwelekeo wetu mkubwa ambao leo tunatoka nao hapa ni HAKIKISHO LA WAKULIMA WOTE WANAOLIMA ALIZETI KWANZA WANATAMBULIKA ILI kuwapatia mbegu bora" 

"Katika msimu huu ni lazima mbegu bora zipatikane na zimfikie kila mkulima ambaye atalima Alizeti msimu huu, hicho ndicho kilimo chenye tija na kilimo ambacho kitaitambulisha Mkoa wa Singida katika kilimo hiki cha alizeti" Amesema Dkt Nchimbi 

Dkt. Nchimbi ametaja mkakati mwingine ni kuhakikisha ununuzi wa Alizeti katika msimu ujao wa kilimo unafanywa na vyama vya Msingi vya Ushirika ili kuondoa au kupunguza tatizo la bei isiyo ya uhakika ya alizeti.

Amesema uzalishaji wa Zao la alizeti ukiongezeka utawezesha Viwanda vilivyopo mkoani Singida kufanya kazi kwa mwaka mzima ambapo kwa sasa viwanda vingi vinafanyakazi katika kipindi cha miezi sita tuu kutokana na kukosa malighafi.

Akizungumzia viwanda, Dkt. Nchimbi amesema kwa sasa mkoa una Viwanda 144 vya kusindika alizeti na vinahitaji zaidi ya tani 595,000 ili kukidhi mahitaji ya Viwanda hivyo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida pia amewasisitiza wakulima kuchangamkia fursa za Mikopo kutoka kwenye Taasisi za kifedha ikiwemo TADB, NMB, CRDB, TPB na Vision Fund.

Kwa upande wao wakulima wa Zao la Alizeti mkoa wa Singida wameziomba Taasisi za kifedha kuwakopesha pembejeo hizo kupitia Taasisi zinazouza pembejeo hizo ili pindi watakapovuna na kuuza Zao hilo la Alizeti waweze kurejesha mikopo hiyo haraka kwani kwa sasa wakulima wengi hawana uwezo wa kununua pembejeo hizo kutokana na pembejeo hizo kuuzwa bei kubwa.

Kwa upande wao Shirika lisilo la Kiserikali FAIDA MALI limeihakikishia Serikali ya mkoa wa Singida kuwa mbegu zote bora za alizeti zinazohitajika kwa Wakulima wote wanaolima Alizeti mkoani Singida zitapatikana kwa msimu huu 2018/2019 na pia wameahidi kujenga magodauni ili kuleta mbegu ndani ya mkoa ili mbegu hizo  zimfikie kirahisi mkulima wa Alizeti.

Mkutano wa Mkakati wa upatikanaji wa mbegu bora za alizeti msimu wa 2018/2019 mkoani Singida ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa RC Social na kuhudhuriwa na waheshimiwa wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri, Mkurugenzi wa Shirika la FAIDA MALI, Wawakilishi wa Makampuni ya wasindikaji wa alizeti, Wawakilishi wa Makampuni ya pembejeo, Wawakilishi wa Vyama vya Ushirika, Wataalamu kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri pamoja na wawakilishi wa Wakulima wa Alizeti. 

MATUKIO KATIKA PICHA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa Mkutano wa Mkakati wa Upatikanaji wa Mbegu Bora za Alizeti Msimu wa 2018/2019 mkoani Singida.


 Washiriki wa mkutano wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani) akizungumza wakati wa Mkutano wa Mkakati wa Upatikanaji wa Mbegu Bora za Alizeti Msimu wa 2018/2019 mkoani Singida.


 Mwakilishi wa Wakulima kutoka Ilongero wilaya ya Singida vijijini akizungumza wakati wa Mkutano wa Mkakati wa Upatikanaji wa Mbegu Bora za Alizeti Msimu wa 2018/2019 mkoani Singida.




 Wauza pembejeo wakizungumza wakati wa Mkutano wa Mkakati wa Upatikanaji wa Mbegu Bora za Alizeti Msimu wa 2018/2019 mkoani Singida.


Mwezeshaji kutoka CRDB Bank akizungumzia fursa za mikopo zilizopo na mpango wa benki katika kuwasaidia wakulima kwa msimu 2018/2019 wakati wa Mkutano wa Mkakati wa Upatikanaji wa Mbegu Bora za Alizeti Msimu wa 2018/2019 mkoani Singida.

Wauza pembejeo wakionyesha Technolojia ya zana bora za kilimo wakati wa Mkutano wa Mkakati wa Upatikanaji wa Mbegu Bora za Alizeti Msimu wa 2018/2019 mkoani Singida.

IMETOLEWA NA;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano 
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 
Singida

No comments:

Post a Comment