Mkuu wa mkoa wa
SINGIDA Dkt. REHEMA NCHIMBI ameagiza magari yote ya Serikali na Mashirika ya
Umma mkoani humo kuanzia sasa yaanze kubeba wanawake wajawazito pindi
wanapohitaji huduma ya dharura ya kujifungua kama eneo hilo halina gari la
kubebea wagonjwa ikiwa ni hatua ya kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na
watoto.
Dkt. Nchimbi ametoa
agizo hilo mapema jana 21/11/2018 katika uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” kufuatia kuendelea kuongezeka kwa vifo vya wanawake wajawazito na
watoto ambapo kati ya mwaka 2014 hadi 2018 jumla ya watoto 3265 walifariki na
katika hicho kipindi wanawake wajawazito 217 walifariki kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo upungufu wa damu.
Mkuu huyo wa mkoa
ameonya kuwa kiongozi yeyote atakaye kwamisha mpango huo wa kupunguza vifo vya watoto
wachanga pamoja na wamama wajawazito mkoani Singida atachukuliwa hatua kali za
kisheria.
“ 3265 ni kijiji
kizima, yani tumekifuta kijiji kizima, tusiruhusu hata kifo kimoja cha mama mjamzito
au mtoto mchanga kwa sababu ambazo
zinaweza kuzuilika, na kama tunaona kuna kituo cha afya au hospitali kuna bigwa
ambaye hatufai katika oparesheni yetu nipeni taalifa ili nishuke naye jumla
jumla” Alisisitiza Dkt Nchimbi
Aidha, viongozi wa
mkoa wa SINGIDA wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa SINGIDA Dkt. Rehema Nchimbi sasa
wamejitwika jukumu la kuhakikisha vifo vya watoto wachanga na wanawake
wajawazito vinakoma.
Katika uzinduzi huo, Wakuu wa wilaya za mkoa wa SINGIDA wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa SINGIDA
wamesaini tamko la kuongeza kasi ya uwajibikaji katika kupunguza vifo
vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga katika kampeni ya JIONGEZE,
TUWAVUSHE SALAMA MANENO BASI SASA NI VITENDO.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mganga mkuu wa mkoa Dkt. Victoria Ludovick akizungumza.
Katibu Tawala Mkoa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza.
Viongozi wa Dini mbalimbali mkoa Singida wakinakili jambo. Kutoka kulia Padri. Festo Kingwai, Askofu Amos Magas FPCT, Hamisi Kisuke mwenyekiti BAKWATA Manispaa ya Singida pamoja na Mkuu wa wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskasi Muragili.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza.
Wakuu wa wilaya za mkoa wa Singida wakinakili jambo. Kutoka kulia Mhe. Emmanuel Luhahula Mkuu wa wilaya ya Iramba, Mhe. Mhandisi Jackson Masaka Mkuu wa wilaya ya Mkalama, Mhe. Miraji J. Mtaturu Mkuu wa wilaya ya Ikungi, na Mhe. Rahabu Mwagisa Mkuu wa wilaya ya Manyoni.
IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA
SINGIDA
No comments:
Post a Comment