MKUU wa mkoa wa
Singida Dkt. Rehema Nchimbi, ameagiza halmashauri zote za wilaya na manispaa
mkoani Singida, kuanzisha madawati yatakayo
simamia mawasiliano kati ya TAREA (Tanzania Renewable
Energy Association) na halmashauri hizo, yatakayohusu upatikanaji na usambazaji
wa nishati mbadala.
Dkt Nchimbi, ametoa wito huo jana wakati
akizindua maonesho ya nishati mbadala ya siku mbili yaliyofanyika
kwenye viwanja vya Peoples klabu mjini hapa. Alisema dawati hilo liwe kwenye ofisi za halmashauri, na
lisimamiwe kikamilifu na maafisa maendeleo ya jamii ili iwe na mawasiliano
endelevu na TAREA.
Katika hatua nyingine, ameziagiza halmashauri hizo kuhakikisha
zinaweka umeme wa nishati mbadala katika shule za msingi, sekondari, mabweni na
vyanzo vya maji.
“Tutumie umeme wa nishati mbadala katika shule zetu, wanafunzi
waweze kutumia mwanga huo kujisomea bila matatizo. Kupitia mwanga huo, wataweza
kuinua taaluma zao na hivyo kufanya vizuri zaidi kwenye mitihani yao” Dkt. Nchimbi.
Dk.Nchimbi alitumia fursa hiyo kukishukru chama cha TAREA, kwa kuleta maonyesho hayo mkoani Singida. Amedai kupitia
maonyesho hayo wananchi watapata elimu na maarifa juu ya umuhimu wa kutumia
nishati mbadala kwenye shughuli mbalimbali zikiwemo za kiuchumi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa TAREA kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo katika manispaa ya Morogoro, Profesa Amini Kweka, alisema TAREA ni chama ambacho kimeundwa na watu mbalimbali na taasisi zisizo za kiserikali zinazovutiwa na malengo ya TAREA.
Alitaja baadhi ya majukumu yao ikiwa ni pamojana
na kueneza maarifa na maelezo juu ya teknolojia za nishati
jadidifu, nakutoa ushauri wa kitaalamu juu ya mambo ya nishati jadidifu, na
kushiriki kuandaa bidhaa zenye viwango bora.
TAREA ni Tanzania Renewable Energy Association, ni jumuiya ya watu ambao wanavutiwa na nishati jadidifu na ambao wanatambua uzuri wa teknolojia za nishati jadidifu (nishati itokanayo na jua, upepo, na maji). TAREA ilisajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani na kupata nambari ya usajiri SA 10900 mnamo tarehe 17 Mei, 2001.
MATUKIO KATIKA PICHA
WASHIRIKI WAKIWA KATIKA ZIARA YA KUTEMBELEA KWENYE MITAMBO YA NISHATI JADIDIFU ITOKANAYO NA JUA PAMOJA NA MTAMBO UNAOSUKUMA MAJI KWA NJIA YA UPEPO KATIKA KIJIJI CHA PUMA NA KIMBWI HALMASHAURI YA IKUNGI MKOANI SINGIDA. 13/10/2018
Imetolewa na;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA
SINGIDA
No comments:
Post a Comment