Thursday, October 11, 2018

VIONGOZI WA NGAZI MBALIMBALI, WANANCHI WASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA BABA MZAZI WA RC KILIMANJARO MHE. ANNA MGWIRA LEO


Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi leo Octoba 11, 2018 ameungana na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama, Taasisi binafsi pamoja na waombolezaji mbalimbali kushiriki mazishi ya Mzee Elisha Mghwira ambaye ni baba mzazi wa Mhe. Anna Mghwira , Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.

Mazishi ya Mzee Elisha Mghwira  ambaye alifariki dunia Octoba 6, 2018 akiwa Jijini Dar es Salaam alipokuwa amepelekwa kwa ajili ya matibabu.

Mazishi  yamefanyika katika makaburi ya nyumbani yaliyopo Kindai Manispaa ya Singida mkoani hapa.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa walioshiriki katika kuomboleza msiba huo na kwa niaba ya viongozi wa Serikali mkoani Singida Dkt. Nchimbi amewasihi wanafamilia  kutumia msiba huo katika kutoa shuhuda kwa mambo mazuri yaliyofanywa na marehemu Mzee Elisha Mghwira  ili kuendeleza na kudumisha umoja na upendo ndani ya familia na kuwaomba waombolezaji walioshiriki katika maombolezo hayo kuondoka na shuhuda mbalimbali zilizoelezwa katika msiba huo.

MATUKIO KATIKA PICHA

 
 

 
 
  'Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe'

IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA
SINGIDA

No comments:

Post a Comment