Saturday, September 01, 2018

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI YAHITIMISHA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI SINGIDA


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. George Simbachawene wakiwasili leo katika ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAO) mkoani Singida.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano  wa ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAO) mkoani Singida.


Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bi. Wendy Massoy akisoma Taarifa katika Kikao na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti inayoongozwa na Mheshimiwa George Simbachawene, kilichofanyika leo katika Ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAO) mkoani Singida

 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George Simbachawene akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo pamoja na viongozi wakuu kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano  wa ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu (NAO) mkoani Singida.

Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. George Simbachawene wakifuatilia kwa umakini taarifa kutoka kwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bi. Wendy Massoy kilichofanyika leo katika Ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAO) mkoani Singida.

Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bi. Wendy Massoy akisisitiza jambo katika Kikao na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, kilichofanyika leo katika Ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAO) mkoani Singida.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George Simbachawene akisisitiza jambo katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano  wa ofisi ya Taifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (NAO) mkoani Singida.

Kikao kikiendelea

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi  akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti mara baada ya kikao kifupi cha mazungumzo na Mkuu wa mkoa Singida.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George Simbachawene akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi  pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti mara baada ya kikao kifupi cha mazungumzo na Mkuu wa mkoa Singida.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George Simbachawene (mwenye suti ya bluu) kulia kwake akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti pamoja na Katibu Tawala Mkoa Singida Dkt. Angelina Lutambi, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Mipango na Uratibu Bw. Barthelomeo Temba (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mkoani Singida.

KAMATI YA BAJETI YATEMBELEA VIWANDA
MKOANI SINGIDA JANA, 31/08/2018
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. George Simbachawene wakikagua maeneo mbalimbali ya hatua za uzalishaji katika Kiwanda cha Mafuta ya Alizeti Mount Meru kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida mkoani Singida. 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. George Simbachawene ilianza ziara yake ya kutembelea Viwanda mkoani Singida jana 31/08/2018 na kuhitimisha leo 01/09/2018 ambapo walitembelea jengo la ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAO-Singida) pamoja na Chuo cha Uhasibu (TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) mkoani Singida. 
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 
Singida

No comments:

Post a Comment