Saturday, September 01, 2018

RC SINGIDA AWAAGIZA WAKURUGENZI NA WAKUU WA WILAYA KUSIMAMIA KWA NGUVU ZOTE MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA UKUSANYAJI WA MAPATO (LGRCIS) ILI KUONGEZA MAKUSANYO NA KUONDOA MIANYA YA UPOTEVU WA MAPATO

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wapili kushoto) akifungua Kikao cha Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu  Mapato na matumizi ya Halmashauri za mkoa wa Singida kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Dkt. Nchimbi amewataka watendaji, viongozi pamoja na watumishi mkoani Singida kuwa mkakati unaoonekana na kuondokana na utendaji kazi wa mazoea na kuwataka watumishi wa halmashauri kuwa na ubunifu unaozihirika ikiwa ni pamoja na kusimamia na kuendeleza ubunifu unaotolewa na baadhi ya viongozi. 


Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akiwasilisha agenda ya Tathimini ya Mapato ya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa mbele ya Wajumbe wakati wa kikao kilichoongozwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.


Katibu Tawala amewasisitiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Mkoa wa Singida kuhakikisha wanaingia kwenye Mfumo wa Mapato (LGRCIS) mara kwa mara na kuhakikisha mashine zote zinazokusanya mapato 'POS' zinaonekana kwenye 'Dashboard' ya Mfumo wa LGRCIS.


 Afisa TEHAMA wa Sekretarieti ya Mkoa wa Singida, Bw. Baraka E. Mhembano akifanya wasilisho juu ya Mfumo wa Mapato - LGRCIS unavyo fanya kazi pamoja na hali ya ukusanyaji wa Mapato katika kila halmashauri mkoani Singida,wakati wa kikao hicho kilichoongozwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Singida. 

Katika kikao hiki muhimu Wajumbe walipitishwa katika Mfumo wa LGRCIS kwa kila Halmashauri na kuona Mashine za kukusanya mapato zinavyoonekana kwenye Mfumo wa LGRCIS, pia  walioneshwa kila Mashine ni lini kwa mara ya mwisho imetuma taarifa zake kwenye mfumo Mkuu.

 Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Singida (mbele) pamoja na wajumbe kutoka halmashauri mbalimbali pamoja na taasisi mbalimbali wakifuatilia kikao cha Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na matumizi ya Halmashauri za mkoa wa Singida kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kulia akizungumza jambo kwa msisitizo   wakati wa Kikao cha Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na  matumizi ya Halmashauri za mkoa wa Singida, kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Singida. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa Singida Dkt. Angelina Lutambi.

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Mbua Chima (wakatikati) pamoja na Wajumbe wengine wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao hicho.

 Waheshimiwa Wenyeviti wa Halmashauri za wilaya za mkoa wa Singida (mbele) pamoja na Wajumbe wengine wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao hicho.

 Kikao kikiendelea.
 
  Kikao kikiendelea.

  Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya mkoani Singida wakiwa wanafuatilia kikao kwa makini.

  Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisisitiza jambo wakati wa kikao.

 Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Bi. Mwajabu Nyamkomola akizungumza wakati wa kikao.

 Mjumbe akichangia mada wakati wa kikao.

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mheshimiwa Miraji J. Mtaturu (kulia) akizungumza wakati wa Kikao cha Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na matumizi ya Halmashauri za mkoa wa Singida kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Singida Vijijini mkoani Singida. 

Aidha Mhe. Mtaturu ametoa wito kwa watumishi kuwa na ushirikiano wa pamoja kati ya halmashauri na halmashauri kwa kuwa na mkakati mahususi wa mawasiliano ili kuwahudumia Wananchi  wa mkoa wa Singida kwa pamoja.

 Mganga Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Victoria Ludovick akiwasilisha Mada ya Hali ya Ujenzi wa Vituo vya Afya wakati wa kikao hicho kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Singida.

 Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza na Wajumbe wakati wa kikao.

 Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akisisitiza jambo kwa Wajumbe wakati wa kikao.

 Uwasilishwaji wa Mada ukiendelea.

   Uwasilishwaji wa Mada ukiendelea.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akionesha Mfumo wa Mapato - LGRCIS unavyofanya kazi  na kuwaagiza Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa Mapato katika Halmashauri zao.

 Kikao kikiendelea

 Katibu Tawala Mkoa Singida akifafanua jamba juu ya Mfumo wa Mapato - LGRCIS wakati wa kikao.


 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini Bw. Elia Digha akizungumza wakati wa kikao.

 Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Pasacas Muragiri akizungumza wakati wa kikao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wapili kushoto) wakati akihairisha Kikao cha Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na matumizi ya Halmashauri za mkoa wa Singida kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Singida Vijijini mkoani Singida.

Imeandaliwa na;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
SINGIDA

No comments:

Post a Comment