Friday, August 31, 2018

WAJUMBE KUTOKA WIZARA YA HABARI NA OFISI YA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI KWA PAMOJA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WASEMAJI WA SERIKALI WAFANYA ZIARA MKOANI SINGIDA.

Katibu Tawala mkoa Singida Dkt. Angelina Lutambi (wakatikati) pamoja na wataalamu wa Sekretarieti ya mkoa Singida wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Wizara ya Habari na ofisi ya msemaji mkuu wa Serikali kwa pamoja na viongozi wa chama cha wasemaji wa Serikali wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa habari na kuangalia utendaji kazi wao kwenye taasisi za umma na Halmashauri mkoani Singida.  

 Katibu Tawala mkoa Singida Dkt. Angelina Lutambi kushoto akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa wakati wa kikao cha ushauri na kujadili utendaji kazi wa Maafisa Habari kwenye Taasisi za Umma na Halmashauri mkoani Singida.
  
  Afisa Uhusiano wa Umma katika  Halmashauri ya mji wa Kibaha Bw. Innocent Byarugaba (kushoto) pamoja na Bw. Gerard Chami ambao ni Wajumbe wa Kamati hiyo, wakifuatilia kikao.
  Katibu Tawala mkoa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza naWajumbe kutoka Wizara ya Habari na ofisi ya msemaji mkuu wa Serikali kwa pamoja na viongozi wa chama cha wasemaji wa Serikali wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa habari na kuangalia utendaji kazi wao kwenye taasisi za umma na Halmashauri mkoani Singida.

Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa (kushoto) pamoja na Sarah Msika wakati wa kikao kikiendelea cha ushauri na kujadili utendaji kazi wa Maafisa Habari kwenye Taasisi za Umma na Halmashauri mkoani Singida.
  
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 
SINGIDA
31/08/2018

No comments:

Post a Comment