Sunday, July 29, 2018

TAARIFA KUHUSU KUAPISHWA KWA WAKUU WA WILAYA WAPYA MKOANI SINGIDA WALIOTEULIWA NA MHE. RAIS MAGUFULI, JANA 28 JULAI, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi, siku ya Jumanne tarehe 31 Julai, 2018 saa 03:00 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Singida Vijijini  atawaapisha Waheshimiwa Wakuu wapya wa Wilaya (Singida na Manyoni)  baada ya jana tarehe 28 Julai, 2018 Mhe. Rais Magufuli kufanya mabadiliko katika safu ya uongozi wa nyadhifa hizo.


Kufuatia mabadiliko hayo safu ya Wakuu wa Wilaya Mkoa wa Singida itakuwa kama ifuatavyo;

1.   Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. RAHABU MWANGISA SOLOMON kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.

2.  Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. PASACAS MURAGIRI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida. Anachukua nafasi ya Bw. ELIAS CHORO JOHN TARIMO.

Mhe. Mkuu wa Mkoa Singida atamuapisha Bw. PASACAS MURAGIRI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida. Bw. PASACAS MURAGIRI anachukua nafasi ya Bw. ELIAS CHORO JOHN TARIMO ambaye amestaafu.

Mhe. Mkuu wa Mkoa Singida atamuapisha Bibi. RAHABU MWANGISA SOLOMON kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.
Tukio la kuapishwa kwa viongozi hawa litarushwa kwenye vyombo vya habari mbalimbali wakati wa taarifa ya habari saa mbili kamili usiku kupitia vyombo vya habari vya Redio na Televisheni pamoja na tovuti rasmi ya Mkoa wa Singida ambayo ni www.singida.go.tz pamoja na habari picha zitarushwa (live) kupitia Blog rasmi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida ambayo ni singidars.blogspot.com 
Imetolewa na;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Singida
29 Julai, 2018


No comments:

Post a Comment