Monday, July 02, 2018

RC SINGIDA AONGOZA MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI IKUNGI, 2 JULAI, 2018


Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameongoza mkutano maalum wa Baraza la waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, kujadili majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2018.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Dkt. Nchimbi ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Ikungi kwa kuwa na Hati Safi na kuwataka watumishi, watendaji pamoja na wataalamu kuendelea kuwatumikia kikamilifu wananchi wao vijijini.

"Hati safi inamaana kwamba, sio tuu taarifa za kwenye makaratasi bali tafsiri yake kubwa ni udhihirisho wa hali halisi kwa yale yanayotekelezwa na halmashauri na ambayo yatadhihirika katika mabadiriko chanya ya maisha ya wananchi" Alisema Dkt Nchimbi 

Aidha, Dkt. Nchimbi amewataka watumishi, watendaji, pamoja  na wataalamu kusimamia kila jambo linalohusu maendeleo ya wananchi wa halmashauri ya Ikungi bila kuangalia itikadi za vyama pamoja na kulinda misitu na kuwasihi waheshimiwa Madiwani kusimamia kwa nguvu zote uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti ovyo unaofanywa kwa ajili ya matumizi ya nishati ya kuni na mkaa.

"Niwaombe, mlinde misitu, msifanye mdhaa wowote na ulinzi wa misitu yetu. Niwaombe waheshimiwa Madiwani tudhibiti sana uchomaji wa mkaa" Dkt. Nchimbi 


Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mhe. Rustika Turuka akitambulisha uongozi mbalimbali uliohudhuria kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.


 Sehemu ya waheshimiwa Madiwani 

 Katibu Tawala Masaidizi Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola akizungumza wakati wa utambulisho katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
  
 Sehemu ya wataalamu, watendaji na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Ikungi Mhe. Ally Mwanga akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.  Mweka hazina Bw. Revocatus Mohabe akisoma agenda za kikao wakati wa  kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

    


Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji J. Mtaturuakizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

  

      Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida. Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje Annamary Kakungulu akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
     
 
   
     
 Makamu Mwenyekiti halmashauri ya Ikungi Abel Richard Suri akimshukuru Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi kwa kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

   Makamu Mwenyekiti halmashauri ya Ikungi Abel Richard Suri akitoa neno la shukrani mara baada ya kuhitimisha kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

 Picha ya pamoja  wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
 
   
KATIKA MATUKIO MENGINE KATIKA PICHA 
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAMISEMI JOSEPHAT KANDEGE AWASALIMIA WATUMISHI, WATENDAJI, WATAALAMU PAMOJA NA MADIWANI MARA BAADA YA KUMALIZA KIKAO CHA BARAZA, WILAYANI IKUNGI MKOA WA SINGIDA.
     Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege kusalimia watumishi, watendaji, wataalamu pamoja na Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

 Waheshimiwa Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi wakimsalimia Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege.

     

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege akiwasalimu  watumishi, watendaji, wataalamu pamoja na Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida

   

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege akizungumza na watumishi, watendaji, wataalamu pamoja na Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 
SINGIDA.

No comments:

Post a Comment