Saturday, June 30, 2018

MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, AZINDUA MRADI WA SINGIDANI COMMERCIAL COMPLEX, MJINI SINGIDA LEO 30 JUNI, 2018


Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amewaagiza watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa -NHC- na Taasisi nyingine za Serikali kuhakikisha pindi wanapojenga majengo mbalimbali yakiwemo ya kibiashara au nyumba za makazi kutumia malighali zinazopatikana kwenye eneo husika ili kukuza uchumi wa wafanyabiashara na kukuza ajira kwa Watanzania.

Waziri Mkuu MAJALIWA ametoa maagizo hayo mjini Singida wakati akizindua jengo la uwekezaji la SINGIDANI lilijengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC ambao ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 3.4.

Uzinduzi wa jengo la kisasa la uwekezaji la SINGIDANI mjini Singida umewavutia wananchi wengi ambao wamefika katika eneo hilo kuja kushuhudia uzinduzi wake ambao umefanywa na Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA.  

Katika hotuba yake ya uzinduzi wa jengo hilo, Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amewaagiza watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC kuhakikisha wanatumia malighali za ujenzi wa majengo yanayopatikana katika eneo husika ili kusaidia kukuza uchumi wa wafanyabiasha na kuongeza ajira kwa wananchi.

Pamoja na Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA kusisitiza kuhusu utunzaji wa majengo yaliyojengwa lakini amesema kuwa lengo la Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha idadi kubwa ya wananchi nchini wanapata makazi bora na kwa bei nafuu kupitia ujenzi unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa nchini. 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI amesema ujenzi wa majengo ya biashara yanayojengwa na NHC hayatauzwa kwa wananchi bali yatakuwa yanapangishwa tu.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa SINGIDA Dtk. REHEMA NCHIMBI amesema mkoa huo upo tayari kutoa maeneo ya kujenga majengo ya uwekezaji na nyumba za makazi bila masharti magumu.

"Jengo hili ni ufunguo kiashiria kuwa Singida hii ni njema sana na iko tayari kuwa rafiki mwenza na mwaminifu wa uwekezaji mkubwa, uwekezaji wa kati na uwekezaji wa msingi kuelekea Singida na Tanzania ya viwanda" Alisema Dkt. Nchimbi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo la kisasa la uwekezaji la SINGIDANI (Singida Commercial Complex), mjini Singida. Wengine ni viongozi mbalimbali wa Serikali. Uzinduzi huo umefanyika leo mjini Singida.Hili ndilo jengo la Biashara la Singidani lililojengwa mkoani Singida na NHC, limefunguliwa rasmi leo 30 Juni, 2018 na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

 

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 
SINGIDA

No comments:

Post a Comment