Tuesday, July 31, 2018

RC SINGIDA DKT. REHEMA NCHIMBI AWAAPISHA WAKUU WAWILI WA WILAYA MKOANI SINGIDA



Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi leo tarehe 31Julai, 2018 amewaapisha wakuu wapya wawili wa Wilaya  walioteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli tarehe 28 Julai, 2018.

Wakuu wa Wilaya walioapishwa leo katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa Singida ni Bw. Pasacas Muragiri ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Singida na Bibi. Rahabu Mwangisa Solomon ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.

Hafla ya kuapishwa kwa wakuu hao wa Wilaya imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji J. Mtaturu,  Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi. Jackson Masaka na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi mbalimbali wa Chama (CCM), Dini, Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali mkoa Singida, Wawekezaii pamoja na Wakuu wa Idara katika Sekretarieti ya Mkoa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wakuu wa wilaya wateule kwenda kuchapa kazi na kutatua kero za wananchi katika wilaya zao huku wakizingatia kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu.

Dkt. Nchimbi pia amewataka kusimamia ukusanyaji mapato (kodi) ya Serikali na matumizi ya fedha na rasilimali nyingine za umma sambamba na kuhakikisha vitendea kazi vipo (POS Machine), pia  kuhakikisha wananchi wapo salama na pia kuhakikisha wananchi wanafanya kazi za uzalishaji mali.

"Sio vizuri kiongozi anakuja halafu wananchi wanalalamikia tunakero flani  tunakero flani  tunakero flani tunakero flani, inamaana sisi hatutoshi wakati sisi tupo, wakuu wa wilaya wapo, nami sitaki kuonekana sitoshi, NINATOSHA" Amesema Dkt. Nchimbi

Dkt. Nchimbi amewasihi wakuu wa wilaya kutosubiri migogoro iwafuate mezani bali kufuata wananchi pale kwenye migogoro kushughulikia haraka iwezekanavyo. 

"Usisubiri migogoro ikufuate mezani, wewe toka na nenda kaiangalie hiyo migogoro ndio utakapoona na kuifahamu katika uasilia wake, jitihada kubwa ya Serikali ya awamu ya tano, ni kuhakikisha migogoro inatoweka kwa wananchi, tusiruhusu migogoro itokee kwa wananchi" amesema Dkt. Nchimbi.

Aidha amewataka wakuu wa Wilaya kusimamia miradi yote inayotekelezwa mkoani Singida na kuiorodhesha miradi yote inayotekelezwa katika wilaya zao pamoja na kuifuatilia kwa kuzingatia tarehe ya kuanza mradi, thamani ya fedha ya mradi, unatarajia kuisha lini? na hatua zake mbalimbali.

"Wakuu wa Wilaya msisubiri taarifa za maandishi, zimetuchelewesha sana, tupate taarifa za makaratasi lakini kikubwa tunataka taarifa za yanayoonekana kwa macho, tusisubiri mpaka mhusika ametuharibia" alisisitiza Dkt. Nchimbi


  Mheshimiwa Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiimba wimbo wa Taifa.


Mheshimiwa Katibu Tawala Mkoa Singida Dkt. Angelina Lutambi akiimba wimbo wa Taifa.




Kiongozi wa Dini ya Kikristo akifungua kwa maombi.

Kiongozi wa Dini ya Kiislamu akifungua kwa Dua.


Kiongozi wa Dini ya Kikristo akifungua kwa maombi.



Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimuapisha Bw. Pasacas Muragiri kuwa Mkuu wa wilaya ya Singida Mjini. 


   Bw. Pasacas Muragiri akiapa mbele ya Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani) kuwa Mkuu wa wilaya ya Singida Mjini. 





 Bibi. Rahabu Mwangisa Solomon akiapa mbele ya Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani) kuwa Mkuu wa wilaya ya Manyoni. 


 Mkuu wa mkoa wa Singida akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bibi. Rahabu Mwangisa Solomon, vitabu vya muongozo na utekelezaji.


 Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bibi. Rahabu Mwangisa Solomon, akisalimiana na wakuu wa wilaya mara baada ya kuapishwa.



 Sehemu ya wakuu wa wilaya mkoa wa Singida


 Mkuu wa wilaya Singida Mjini Bw. Pasacas Muragiri(kushoto) pamoja na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bibi. Rahabu Mwangisa Solomon, wakifuatilia hotuba wakati Mkuu wa mkoa Dkt. Nchimbi akihutubia (hayupo pichani).




 Mkuu wa mkoa wa Singida akizungumza na wakuu wa wilaya mara baada ya kuwaapisha.






  Mhe. Mkuu wa mkoa wa Singida akizungumza mara baada ya kuwaapisha wakuu wawili wa wilaya.


  Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akishangazwa na baadhi ya uchafu unaofanya na Night Club zilizopo jirani na maeneo ya shule mkoani Singida.

 Mheshimiwa Katibu Tawala Mkoa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza jambo wakati wa hafla ya kuapishwa kwa wakuu wa wilaya wa Manyoni na Singida Mjini.


  Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye skafu), na kutoka kulia ni Katibu Tawala Mkoa Dkt. Angelina Lutambi, Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bibi. Rahabu Mwangisa Solomon, Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula, Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji J. Mtaturu, Mkuu wa wilaya ya Singida Mjini Bw. Pasacas Muragiri, Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi  Jackson Masaka na Katibu wa CCM mkoa Singida Bw. Jimson Mhagama wakiwa katika picha ya pamoja.

 Viongozi wa Dini mbalimbali mkoa wa Singida (waliosimama) wakiwa katika picha ya pamoja.


 Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Singida (waliosimama) wakiwa katika picha ya pamoja.


 Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida (waliosimama) wakiwa katika picha ya pamoja.





 Kamati ya Ulinzi na Usalama za wilayani Singida (waliosimama) wakiwa katika picha ya pamoja.






 Waandishi wa habari mkoa wa Singida kutoka vyombo mbalimbali vya habari  (waliosimama) wakiwa katika picha ya pamoja


 MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA










Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 
SINGIDA
31 JULAI, 2018.

No comments:

Post a Comment