Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Itigi
mara baada ya kuzungumza nao na kuzindua barabara Manyoni-Itigi-Chaya, ambapo
pamoja na mambo mengine ameagiza ujenzi wa barabara ya Chaya-Nyaua yenye
kilomita 85 na ujenzi uanze ndani ya siku 45 ili barabara hiyo ikamilike kwa
kiwango cha lami.
#Leo tuomboleza kumbukumbu za Mashujaa, tumeamua
kufanya Maadhimisho hayo kwa kusaidia shughuli za kijamii- Rais Dkt. Magufuli.
#Mkoa wa Singida ulikuwa na KM 3 tu za barabara za
lami, lakini leo una KM 495 za barabara za lami - Rais Dkt. Magufululi.
#KM 495 nimezishiriki kuzijenga nikiwa Waziri wa
Ujenzi - Rais Dkt. Magufuli.
#Tangu nimeanza ziara yangu Biharamuro mpaka hapa
Itigi, nimezindua zaidi ya KM 707 za barabara za lami zenye thamani ya zaidi ya
Bil. 860 - Rais Dkt. Magufulu.
#Fedha zote za ujenzi wa barabara hizo zimetolewa
na Serikali kwa asilimia 100 - Rais Dkt.
Magufuli.
#Tumeamua kulipa malimbikizo ya madeni ya wakandarasi zaidi ya Tsh. Tril. 1 - Rais Dkt. Magufuli.
#Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Afrika
zilizotoa umeme 45% kwa wananchi wake - Rais Dkt. Magufuli.
#Itigi wala Manyoni hapakuwa na umeme, lakini leo
wana umeme - Rais Dkt. Magufuli.
#Tunataka tuwe na umeme wa uhakika ili Tanzania ya
viwanda ifanikiwe - Rais Dkt. Magufuli.
#Ndoto ya Baba wa Taifa ya kuifanya Dodoma kuwa
Makao Makuu ya Nchi lazima tuitimize kwa vitendo - Rais Dkt. Magufuli.
#Zaidi ya Watumishi 3000 wameshahamia Dodoma -
Rais Dkt. Magufuli.
#Makao Makuu yakishakuwa Dodoma inamaana na miji
ya karibu nayo itakuwa kama Makao Makuu ya Nchi - Rais Dkt. Magufuli.
#Wakati wa kukaa kwenye magenge na kusikiliza
maneno kwamba mtaletewa vya bure umeshapita - Rais Dkt. Magufuli.
#Nataka niwatendee Watanzania haki na kuwaeleza
kweli - Rais Dkt. Magufuli.
#Ndio maana nawaambia Watanzania kwamba Tanzania
tumeibiwa vya kutosha - Rais Dkt. Magufuli.
#Nataka niijenge Tanzania mpya - Rais Dkt.
Magufuli.
#Mimi ni CCM lakini nafanya kazi za Watanzani
wote, sibagui - Dkt. Magufuli.
#Mwaka huu tumetangaza nafasi 50 elfu za manesi,
madaktari na walimu - Rais Dkt. Magufuli.
# Ajira zilikuwa hazitangazwi kutokana na ajira
kuzibwa na wafanyakazi hewa zaidi ya 19,000 - Rais Dkt. Magufuli.
#Tanzania tunajenga Reli ya aina yake Afrika nzima
ambayo itatumia umeme - Rais Dkt. Magufuli.
#Nataka Tanzania iwe ya kisasa - Rais Dkt.
Magufuli.
#Tukishakuwa na miundombinu ya lami, nchi itatajirika kutokana na biashara
zitakazofanyika - Rais Dkt. Magufuli.
#Tanzania ni kati nchi 5 Afrika zinazokuwa kwa
kasi kiuchumi, ambapo Tanzania inakua kwa 7% - Rais Dkt. Magufuli.
#Ndugu zangu wa Itigi tuanze kulima Uwele, Mtama,
Viazi na Mihogo ambavyo vinastahimili mvua kidogo - Rais Dkt. Magufuli.
#Tumefuta tozo zaidi ya 80 kwenye kilimo - Rais
Dkt. Magufuli.
#Tumefuta zaidi ya tozo 7 kwenye mifugo na zaidi
ya tozo 5 kwenye uvuvi - Rais Dkt. Magufuli.
*Imeandaliwa na Idara ya Habari - MAELEZO.*
No comments:
Post a Comment