Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi
(anayeangalia kamera) akimpatia Nya Mathias shilingi 34,500 kama malipo ya kuchimba
bwawa kwa siku 15 ambapo kila siku anapaswa kulipwa shilingi 2,300. Fedha hizo
zimetolewa na TASAF 111 kwa ajili ya kunusuru kaya maskini kupitia miradi ya
jamii iliyoibuliwa na walengwa wa TASAF.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiangalia
bwawa linaloendelea kuchimbwa na kaya maskini za kijiji cha Kikonge wilaya ya
Iramba kupitia TASAF 111. Mkuu huyo wa mkoa ameagiza halmashauri zote zisaidie
kutoa fedha ili ujenzi wa mabwawa yaliyoibuliwa na kaya masikini yaweze kukamilika
kwa muda mfupi.
Na Gasper Andrew- Singida.
Mkuu wa
Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameagiza maafisa mifugo kata
kusimamia kwa karibu miradi ya ufugaji kuku na mbuzi inayotekelezwa na kaya
maskini zilizopo kwenye mpango wa TASAF 111.
Amesema
kuku au mbuzi katika miradi hiyo wakifa kwa kukosa huduma kutoka kwa maafisa
mifugo,maafisa hao watalazimika kufidia kuku au mbuzi hao watakaokufa.
Akilijengea
nguvu agizo lake hilo Dkt. Nchimbi alitoa kutoka mfukoni kwake shilingi 150,000
taslimu na kumpatia afisa mifugo kata ya Kikonge Wilayani Iramba kwa ajili ya
kuikarabati pikipiki yake iweze kumrahihishia kufika kwenye miradi ya kaya
maskini.
Dkt.
Nchimbi ametoa agizo hilo juzi muda mfupi baada ya kumaliza kukagua bwawa la
kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba linalojengwa kwa nguvu za kaya maskini.
Amesema
serikali pamoja na wadau wanaotoa fedha kwa kaya maskini,ili ,ziweze kujikwamua
kutoka lindi la umaskini.
“Njia
mojawapo ya kuzisaidia kaya hizi maskini kuboresha vipato vyao,ni hii ya miradi
midogo midogo ya ufugaji kuku,mbuzi na mifugo meinge.Ninyi maafisa mifugo
ambao mpo karibu na kaya hizi,zisimamieni kikamilifu,msisubiri mfuatwa,ninyi
ndio muifuate miradi huko iliko”,alisisitiza.
Aidha,
mkuu huyo wa mkoa, amewataka watendaji hao wahakikishe wana simamia
watoto wa kaya maskini wana hudhuria shuleni bila kukosa.
“Serikali
inaamini hawa watoto wa kaya maskini ambao TASAF inagharamia masomo yao, ndiyo
watakao kuja kuwa mtaji kwa kaya maskini kujikomboa kiuchumi. Kwa hiyo upo
umuhimu mkubwa wa kusimamimiwa na kuhimizwa kusoma kwa bidii”,alifafanua.
Mkuu
huyo wa mkoa, pia amewataka walimu watambue kwamba wana fundisha watoto ambao
wengine wakiwa ni wa kaya maskini,.Kwa hali hiyo, mchango wao unatakiwa
katika kuwa jengea misingi itakayo weza kusaidia kuzikomboa kiuchumi kaya
zao.
Awali
mratibu TASAF mkoa wa Singida, Patrick Kasango, alisema mpango wa
kunusuru kaya maskini (PSSN) unatekelezwa na TASAF 111, katika wilaya
zote sita za mkoa huu.
Alisema
mpango huo ulianza na kaya 39,426, lakini kutokana na sabaubu mbalimbali hadi
sasa zimebaki kaya lengwa 39,102.
“kaya
hizi maskini zimewezeshwa kupata mahita ya msingi ikiwemo chakula hasa
wakati wa njaa, mahudhurio shuleni yameboresha kwa wanafunzi na kuboresha afya
za watoto wadogo wanaodhuziria kliniki.Kwa kifupi,hadi januari mwaka huu,
zaidi ya shilingi 20.3 bilioni, zimehawilishwa kwa kaya masikini
mkoani kwetu”,alisema Kasango.
Wakati
huo huo Mmoja wa wanaufaikaji wa mpango huo wa TASAF 111,Elizabeth
Mkumbo,amesema amefanikiwa kujenga nyumba bora,kuwa na akiba na kuanzisha
ufugaji wa kuku kupitia fedha za mradi wa TASAF 111.
Mkazi wa kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba Mkoani
Singida Stephano Mkiya akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la kuhaulisha
fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini amesema kupitia fedha za TASAF ameweza
kuanzisha ufugaji wa mbuzi na pia anamudu kuwasomesha watoto wake.
Mkazi wa kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba Mkoani
Singida Elizabeth Mkumbo akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la kuhaulisha fedha
za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini, Elizabeth amesema kupitia fedha za TASAF
ameweza kujenga nyumba bora ya mabati na kwa sasa ana uhakika wa chakula tofauti
na kipindi hajaunganishwa na mpango wa TASAF.
Mratibu wa TASAF Mkoani Singida Patrick G. Kasango akizungumza
muda mfupi kabla ya zoezi la uhaulishaji wa fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya
maskini 146 katika kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba mkoani hapa. Kwa mujibu wa
Kasango hadi sasa kaya 39,102 maskini Mkoa wa Singida zimenufaika kwa kupatiwa
zaidi ya shilingi bilioni 20.3.
No comments:
Post a Comment