Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi akipanda viazi lishe katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama katika ziara yake wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Jakson Masaka akishiri kupanda viazi lishe katika shamba la Mkulima katika kijiji cha Nkungi Wilayani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akipanda viazi lishe
katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani
Mkalama.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi au “mama Nchimbi” kama anavyojulikana jana
amefanya ziara ya kikazi Wilaya ya Mkalama na kuagiza watendaji kusimamia
miradi kwa umakini kwakuwa hataki kusikia mradi wowote uko chini ya kiwango.
Dkt. Nchimbi amesema
msamiati chini ya kiwango hataki kuusikia kwakuwa umekua ukifanya watendaji
kuwa wazembe na kuongeza kuwa hatua kali zitachukulkiwa kwa viongozi wote ambao
hawatasimamia ipasavyo utekelezaji wa maelekezo hayo.
Ameongeza kuwa
watendaji wamekuwa wakiilalamikia serikali na kuirudisha nyuma kwa kutotekeleza
majukumu yao ipasavyo na hivyo kupelekea wananchi kuona serikali haifanyi
chochote wakati inaleta pesa nyingi za miradi mbalimbali ambapo jukumu la
watumishi ni kusimamia miradi ili ifanye kazi ipasavyo.
Dkt. Nchimbi amesema
viongozi wote kabla ya kusaini mikataba yoyote ya halmashauri wanapaswa kukiri
thamani ya mali zao zinazohamishika na zisizohamishika ili kama mradi
utatekelezwa chini ya kiwango, mali zao zitumike kufidia pesa ya serikali
iliyopotea.
“Mradi wakati
unajengwa Mkurugenzi, Mwenyekiti wa halmashauri na wataalam wanauangalia bila
kusema chochote, ukikamilika ndio wanakuambia umejengwa chini ya kiwango,
kuanzia sasa sitaki kusikia msamiati wa ‘chini ya kiwango’ na endapo ikitokea
chini ya kiwango tutahakikisha fedha ya serikali inarudi", amesema Dkt. Nchimbi.
Aidha katika kikao
hicho na watumishi wote wa halmashauri hiyo amewaagiza wakuu wote wa shule za
msingi na sekondari kuwaruhusu wanafunzi ambao hawana sare kuanza masomo huku utaratibu
wa kuwafuatilia wazazi watimize majukumu yao ukiendelea.
“ Baada ya elimu kuanza kutolewa bure,
changamoto nyingine iliyobakia kwa baadhi ya wazazi ni uwezo wa kuwashonea
watoto wao sare za shule, sasa ninaagiza wakuu wa shule za sekondari na Msingi
wote Wilayani hapa kuwaruhusu watoto hao waingine madarasani hata kama
hawajavaa sare za shule ili wasikose haki yao ya msingi kwa sababu ya sare tu”,
ameagiza Dkt. Nchimbi.
Awali kabla ya
kuzungumza na watumishi Dkt. Nchimbi alifanya ziara katika mashamba ya wakulima
ili kujionea na kushiriki na wananchi shughuli za kilimo hasa mashamba ya viazi
katika kijiji cha Nkungi na mashamba ya mtama katika kijiji cha Ilunda wilayani
humo.
Dkt. Nchimbi akiwa
katika shamba la mkulima wa viazi lishe katika kijiji cha Nkungi alipanda viazi
na kuhamasisha wananchi wengine walime mazao ambayo yanatumia maji kwa ufanisi
kama vile viazi, mihogo, matama na uwele kutoka na mabadilike ya tabia nchini
ili kujihakikishia uwepo wa chakula.
Amewataka watendaji
hasa wa kada za kilimo na ufugaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea hasa kuandaa
taarifa za makaratasi bali wawatembelee wakulima na wafugaji katika maeneo
wanayofanya shughuli zao ili waweze kutoa ushauri kwa kupata picha halisi.
“Sipendi kiongozi
anayesema yupo karibu na wananchi kwa sababu hatuwezi kupima ukaribu uliopo
hivyo ni vyema kuanzia sasa tuache kuwa karibu na badala yake tuwe pamoja nao”,
amesema Dkt. Nchimbi.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akisadiniana na mkulima kuandaa matuta kwa ajili ya kupanda viazi lishe
katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani
Mkalama.
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Mklama wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao juu ya uadilifu na kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya hapa kazi tu.
No comments:
Post a Comment