Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. Mwigullu Lameck Nchemba akiwa katika kikao cha 38 cha bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mwenyekiti wa Bodi ya barabara Mkoani hapa Mhandisi Mathew John Mtibumwe akiendesha kikao cha 38 cha bodi ya barabara ya Mkoani hapa, Kulia kwake ni Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Mhe, Martha Mlata.
Meneja wa TANROADS Mkoani Singida Mhandisi Leonard Kapongo akijibu baadhi ya hoja katika kikao cha 38 cha bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida.
Wajumbe na wadau mbalimbali wa bodi ya barabara wakichangia hoja katika kikao cha 38 cha bodi ya barabara ya Mkoa wa
Singida.
Na Nathaniel Limu
Waziri
wa mambo ya ndani Mhe. Mwigullu Lameck Nchemba (mb), ameliagiza jeshi la polisi
nchini,kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria madereva wanaoacha
mawe na matawi ya miti barabarani.
Nchemba
ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iramba mkoani Singida, ametoa agizo hilo
wakati akizungumza kwenye kikao cha 38 cha bodi ya barabara mkoa kilichofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.
Amesema
baadhi ya madereva wa magari na hasa yale makubwa,hutumia mawe kuzuia magari
yao kutembea wakati wakiyafanyia matengenezo ya dharura.
“Wakiisha
maliza kuyafanyia matengenezo magari yao, madereva hao huyaacha barabarani mawe
na matawi ya miti ambayo hutumika kutoa tahadhari kwa vyombo vingine vya moto. Kitendo
hicho kinahatarisha maisha na mali za watumiaji wengine wa barabara kwa vile
yanaweza kusababisha ajali”, amesema Mwigullu.
Kwa
hali hiyo amesema jeshi la polisi linapaswa kuimarisha mawasiliano ili waweze
kuwathibiti na kuwakamata madereva wanaoacha mawe na matawi ya miti barabarani.
Katika
hatua nyingine, waziri huyo amesema upo umuhimu mkubwa wa wananchi na hasa wale
wanaoishi kando kando ya barabara kuelimishwa juu ya matumizi bora ya barabara
zinazojengwa kwa fedha nyingi ili waweze kuacha kupitisha mifugo yao na
mikokoteni barabarani.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa bodi ya barabara na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi
Mathew John Mtigumwe ameagiza kuwa fedha zinazotolewa na serikali na wafadhili
mbalimbali wa miradi ya barabara matumizi yake yasimamiwe kikamilifu, ili
zitumike kwa miradi iliyokusudiwa.
“Ujenzi
wa miradi hiyo ya barabara ufanane na thamani halisi ya fedha zilizotumika. Pia
kazi za ujenzi wa barabara za ngazi zote wapewe wakandarasi bora na wenye uwezo
wa kutekeleza miradi ikakamilika kwa wakati. Nasisitiza kuimarishwa kwa
usimamizi na ukaguzi wa mara kwa mara wa miradi ya barabara ili ziwe za kiwango
kinachokusudiwa”,amesema.
Wakati
huo huo, mhandisi Mtigumwe ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa alikuwa
meneja TANROADS mkoa, ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa TANROADS mkoa
wa Singida chini ya meneja wake Mhandisi Leonard Kapongo kwa kazi nzuri ya usimamizi
na ukaguzi uliopelekea miradi ya barabara kujengwa kwa ubora unaofafana na
fedha zilizotumika.
No comments:
Post a Comment