Daktari bingwa wa macho Mkoani Singida Ngh'ungu Kuzenza akimfanyia uchnguzi wa macho mgonjwa wa kisukari katika kuadhimisha siku ya kisukari duniani.
Baadhi ya wagonjwa wa kisukari wa kliniki ya Hospitali ya Mkoa wa Singida wakisubiria kufanyiwa uchunguzi wa macho katika kuadhimisha siku ya
kisukari duniani.
Wagonjwa wa kisukari Mkoani
Singida leo wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya macho na daktari bingwa wa
macho katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa kisukari duniani ikiwa na kauli
mbiu ya ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya macho.
Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida Dokta Ramadhani Kabala amewaambia wagonjwa
wa kisukari waliohudhuria kufanyiwa uchunguzi wa macho kuwa maadhimisho hayo mwaka
huu yamelenga kuzuia wagonjwa wasiathirike zaidi na magonjwa yatokanayo
kisukari.
Dokta Kabala amesema
ugonjwa wa kisukari hushambulia zaidi macho, figo na moyo hivyo serikali
imeweka mkazo wa kuwafanyia uchunguzi ili kubaini tatizo ili wapatiwe matibabu
mapema au kuzuia yasitokee kabisa kwa kufuata kanuni na taratibu za ugonjwa huo.
Ameongeza kuwa
ugonjwa wa kisukari unawakumbusha watu kuishi kwa kufuata kanuni bora za afya
kama kula mlo kamili, kula matunda badala ya juisi zilizotengenezwa viwandani,
kufanya mazoezi na kupunguza vilevi na sigara hivyo wagonjwa wa kisukari hawana
togauti na watu wengine isipokuwa wao hushauriwa kufuata kanuni hizo kwa
umakini mkubwa.
Dokta Kabala
amewakumbusha kutumia dawa kwa kufuata usahuri wa daktari wao pamoja na
kuhudhuria kliniki za kisukari kwakuwa kliniki hizo zinawasaidia katika
kushauriana namna bora ya kuishi kwa kufuata masharti wananyopewa pamoja kuelimishanzaidi
juu ya ugonjwa huo.
Naye Daktari bongwa
wa macho Mkoani Singida Dokta Ngh’ungu Kuzenza amesema utaratibu huo unasaidia
kuzuia au kupunguza madhara ya ugonjwa wa kisukari kwakuwa wengi watatambuliwa
kabla hawajafikia hatua ya kupofuka.
Dokta Kuzenza
ameongeza kuwa changamoto kubwa ni watu wengi kutopima ugonjwa wa kisukari
mapema mpaka wanapougua na hivyo kujikuta wameshaathirika macho ndipo hutafuta
huduma.
Kwa upande wake mmoja
kati ya wagonjwa wa kisukari 76 waliopata huduma ya kibingwa ya macho Bi Asha
Selemani Waziri Mkazi wa Iguguno ameema serikali imeweka utaratibu mzuri wa
kuwapima macho ili waweze kupata tiba mapema.
Bi Waziri ameiomba
serikali kuendelea kuweka utaratibu wa kuwapima wagonjwa wa kisukari magonjwa
mbalimbali kama moyo na figo huku akiwashauri wagonjwa wa kisukari kufuata
ushauri wanaopewa na wataalamu wa afya.
Daktari bingwa wa macho Mkoani Singida Ngh'ungu Kuzenza akimfanyia
uchnguzi wa macho mgonjwa wa kisukari katika kuadhimisha siku ya
kisukari duniani.
Baadhi ya wagonjwa wa kisukari wa kliniki ya Hospitali ya Mkoa wa
Singida wakisubiria kufanyiwa uchunguzi wa macho katika kuadhimisha
siku ya
kisukari duniani.
No comments:
Post a Comment