Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe akipata maelezo kuhusu kitengo cha huduma ya watoto mahututi (Neonatal Intensive care unit) katika hospitali ya Kiomboi Wilayani Iramba.
Mkurugenzi wa Shirika la Water Aid Tanzania uu
wa Dokta Ibrahim Kabole akipata
maelezo kuhusu kitengo cha huduma ya watoto mahututi (Neonatal Intensive
care unit) katika hospitali ya Kiomboi Wilayani Iramba.
Mwakilishi wa Shirika la Water Aid International akipata
maelezo kuhusu kitengo cha huduma ya watoto mahututi (Neonatal Intensive
care unit) katika hospitali ya Kiomboi Wilayani Iramba, pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba Dokta Boniphace Richard.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe ameipongeza hospitali ya Kiomboi
ambayo ni ya Wilaya ya Iramba kwa kupata hadhi ya nyota mbili kutoka sifuri na
kuwahamasisha kuendelea kuboresha utendaji ili kupata hadhi ya nyota tatu.
Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe
ametoa pongezi hizo alipotembelea hospitali hiyo akiambatana na wageni kutoka
shirika la Water Aid International ambalo limefadhili ukarabati wa miundombinu
hospitalini hapo kwa shilingi milioni mia tano kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Amesema hospitali
ikiwa na hadhi ya nyota tatu itasaidiwa na serikali pamoja na wadau mbalimbali katika
kuipatia wataalamu zaidi, kuboreshewa zaidi miundombinu, kuwekwa katika mipango
ya kitaifa pamoja na kupata fedha zaidi.
Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe
ameongeza kuwa kutokana na kuboreka kwa huduma za hospitali ya Kiomboi wagonjwa
wameongezeka sana na hivyo ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na
halmashauri ya Wilaya ya Iramba inaboresha Vituo vya Afya vya Mgongo na Ndago
ili vituo huduma za zarudha za Mama na mototo kwa kufanya upasuaji na hivyo kupunguza
msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Kiomboi.
Naye Mkurugenzi wa
shirika la Water Aid Tanzania Dokta Ibrahim Kabole ameshukuru ushirikiano
wanaoupata kutoka kwa watendaji wa wilaya ya Kiomboi hadi kufanikisha ujenzi na
ukarabati wa miundombinu ya hospitali ya Kiomboi huku akiwataka kuitunza na
kuendeleza pale shirika hilo lilipoishia.
Dokta Kabole amesema
shirika hilo limekarabati wodi ya wazazi wanaosubiria kujifungua, kuweka
miundombinu ya maji na matenki, kujenga kichomea taka kipya chenye hadi ya
kisasa hospitalini hapo, kununua friji ya kuhifadhia damu katika kituo cha acya
cha ndago na kutoa mafunzo kwa watoa huduma.
Ameongeza kuwa
shirika hilo litaendelea kushirikiana na viongozi wa Mkoa wa Singida katika
kuboresha sekta ya afya mkoani hapa hasa katika kuboresha afya ya mama na mtoto.
Naye Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Kiomboi Dokta Boniphace Richard ameishukuru Water Aid na kuongeza
kuwa imesaidia hospitali hiyo kupata hadhi ya nyota mbili kutoka sifuri kutokana
na kuboreshwa kwa miundombinu ya hospitali hiyo.
Dokta Richard amesema
Wodi iliyoboreshwa na shirika hilo kwa sasa inapokea wakina mama wanaosubiria
kujifungua 50 ambapo awali walikuwa wana uwezo wa kulaza 30 kwa siku, maji
yanahifadhiwa lita 4500 ambazo zinasadia akina mama hao pamoja na uendeshaji wa
shughuli nyingine za hospitalini hapo, kupungua kwa vifo vya akina mama kwa
asilimia 30.
Ameongeza kuwa
uboreshaji wa miundombinu hospitalini hapo kumepelekea kuanzishwa kwa kitengo
cha Watoto mahututi katika wodi ya wazazi (Neonatal Intensive care unit), ambapo
watoto wanaozaliwa na matatizo mbalimbali wanapatiwa huduma hapo na kuokolewa
maisha tofauti na awali.
Mwakilishi wa Shirika la Water Aid International akiangalia akinamama wanaosubiri kujifungua wakichota maji, miundombinu ya maji imekarabatiwa na shirika hilo wakishirikiana na shirika la SEMA Tanzania.
Akina mama wanaosubiria kujifungua wakiwa nje ya wodi ya kusubiria iliyokarabatiwa kwa ufadhili wa shirika la Water Aid wakishirikiana na shirika la SEMA Tanzania.
Matenki ya maji yaliyokarabatiwa na Shirika la Water Aid International kwa ushirikiano na shirika la SEMA Tanzania.
Jengo la mbele ni Kichomea taka cha zamani na nyuma yake ni jengo jeupe jipya ni kichomea taka kipya na cha kisasa kilichojengwa na Shirika la Water Aid International kwa ushirikiano na shirika la SEMA Tanzania.
No comments:
Post a Comment