Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza na wakazi wa Ilongero, pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe amemtaka Mkuu wa
Wilaya ya Singida kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya kuhamishia makao makuu ya
halmashauri ya Singida katika mji mdogo wa Ilongero ndani ya kipindi cha miezi
sita ili kusogeza huduma karibu na wananchi wa halmashauri hiyo.
Mheshimiwa
Mhandisi Mtigumwe amefikia uamuzi huo kutokana na taarifa za kuwepo watu
wachache wanaotaka kufanya mabadiliko ya makao makuu bila ya kusikiliza mawazo
ya wananchi wengi huku wananchi wakipendelea makao makuu ya halmashauri hiyo
kuwa katika mji mdogo wa Ilongero.
Ameongeza
kuwa baraza la madiwani la halmashauri ya Singida linapaswa kuketi tena na
kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya wananchi wengi huku akiongeza kuwa endapo
wanataka kufanya mabadiliko wayafanye wakiwa tayari wameshahamia katika
halmashauri yao tofauti na sasa ambapo bado ofisi zipo manispaa ya Singida.
Mheshimiwa
Mhandisi Mtigumwe amesema wananchi wanataka kupatiwa huduma kwa ukaribu hivyo
halmashauri kuhamishiwa Ilongero itasaidia kusogeza Huduma ambapo zitatolewa
kwa ufanisi huku akimshauri Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kujipanga ndani ya
kipindi hicho waanze kutumia ofisi chache zilizopo.
Aidha
Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amewataka wananchi wa halmashauri na Mkoa mzima wa
Singida kujituma na kufanya kazi kwa bidii, wakulima wajiandae FEMA kwa msimu
huu wa kilimo na kujitahidi kutunza vyakula ili kujiepusha na njaa na
wafanyabiashara watumie fursa mbalimbali kujiongezea kipato.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Martha Mlata amesema
chama hicho mkono mapendekezo ya wananchi yakutaka makao makuu kuwa katika
mji mdogo wa Ilongero na kuahidi kufuatilia na kusimamia utekelezaji wake.
Katika
kuunga mkono mapendekezo ya wananchi Mbunge wa jumbo la Singida kaskazini la
kaskazini Mhe. Lazaro Nyalandu amesema kufikia mwezi Januari ataweka ofisi za
Mbunge katika mji wa ili wananchi wapate Huduma na kumfikishia kero kwa
ukaribu zaidi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Mheshimiwa Martha Mlata akizungumza na wakazi wa Ilongero.
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mheshimiwa Lazaro Nyalandu akizungumza na wananchi wa Ilongero.
No comments:
Post a Comment