Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Geoffrey Mwambe akipokea mifuko ya simenti 73 kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawil la Manyoni Bwana Richard Karata.
Na Veronica-Manyoni
Benki
ya CRDB tawi la Manyoni imetoa mifuko 73 ya saruji yenye thamani ya Sh. Mil 1,168,000
ili kuchangia ujenzi wa bweni la Wasichana wa kidato cha tano na sita la Mwanzi
Sekondari iliyopo Wilayani Manyoni, Mkoani Singida lililoteketea kwa moto mwezi
Septemba.
Meneja tawi la
CRDB Manyoni Bw. Richard Karata Mchango huo amewasilisha mchango huo jana
ambapo mchango huo umetolewa na Watumishi wa Benki ya CRDB tawi la Manyoni
walioguswa na tatizo la wanafunzi wa Kidato cha tano na sita wa Mwanzi
Sekondari wanaoishi katika mazingira magumu kwa kukosa bweni.
Msaada huo umepokelewa
na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Geoffrey Idelphonce Mwambe ambaye
amewashukuru sana wafanyakazi hao kwa kujitolea katika kusaidia sekta ya elimu
katika ujenzi wa bweni lililoteketea kwa moto.
“Nawaomba
wananchi na wadau wengine wa maendeleo waendelee kutuunga mkono katika juhudi
za ujenzi wa bweni hili la wasichana wa Mwanzi Sekondari ili waepukane na adha
wanayoipata sasa”, ameongeza Mhe. Mwambe.
Bweni la
Wasichana wa Shule ya Sekondari Mwanzi Wilayani Manyoni liliteketea kwa moto
usiku wa tarehe 9 Septemba, 2016 na kuwaacha Wanafunzi hao wakiwa hawana mahali
pa kulala.
No comments:
Post a Comment