Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe akifungua mkutano wa wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi.
Wananchi wameaswa
kutoa ushirikiano kwa wataalamu watakaofanya utafiti wa viashiria vya ukimwi
utakaofanyika nchi nzima na kuhusisha kaya elfu 16 na kuwafikia watanzania elfu
42,000 wakiwemo watoto elfu nane.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano
cha shirika la ICAP-Tanzania linalofadhili utafiti wa viashiria na matokeo ya
Ukimwi Mama Mihayo M Bupamba amesema utafiti umepokelewa kwa hisia tofauti
ukipotoswa kuwa utahusika kila kaya wakati sio kweli.
Mama Mihayo amesema
utafiti utahusisha kaya chache tu za Tanzania nzima ambapo ambapo kaya hizo zitaombwa
ridhaa na utafiti utafanyika kwa usiri na kufuata sera na taratibu za wizara ya
afya, mila, desturi, usiri na utaalamu wa hali ya juu utazingatiwa hivyo wasiwe
na wasiwasi.
Ameongeza kuwa lengo
utafiti huo ni kuendleza utafiti wa kuoima hali ya ukimwi kila baada ya miaka mine
ambapoa mara ya wisho ulifanyika mwaka 2012.
Mama Mihayo amesema utafiti
huu utahusisha hali ya ukimwi, maambukizi mapya, wingi wa kinga ya mwili, wingi
wa virusi vya ukimwi kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virus vya ukimwi, Uwezo
wa mwili wa kumeng’enya dawa za kupunguza makali pamoja na magonjwa ya kaswende
na homa ya ini.
Ameongeza kuwa
utafiti utasaidia kupata taarifa sahihi kwakuwa nyingi zimekuwa zikipatikana
kwa wale tu wanaoenda kupima hospitali hasa wajawazito au wagonjwa bila
kuhusisha ambao hawajafika kupima.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amesema utafiti ni wa muhimu sana na kuwasihi
wananchi wa Mkoa wa Singida kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wataalamu hao.
Mhandisi Mtigumwe
amesema utafiti huo utasaidia watunga sera waweze kupanga kupanga mikakati
mizuri zaidi ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi.
Ameongeza kuwa
utafiti huo ni wa kipekee kwakuwa utahusisha rika zote tofauti na tafiti
zilizotangulia pia utahusisha vipimo vingi na majibu kutolewa hapohapo.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka shirika la Icap Mama Mihayo Bupamba akitoa mada katika kikao cha wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi.
Wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi wakisikiliza kwa umakini kikao cha utafiti huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe (katikati) akifuatilia mada katika mkutano wa wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi kushoto kwake ni katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu Buhacha B. Kichinda na Kulia kwake ni Kaimu Meneja wa ofisi ya Takwimu Mkoa wa Singida Naing'oya Kipuyo.
No comments:
Post a Comment