Wednesday, September 07, 2016

WANAFUNZI ELFU 21 WAANZA MITIHANI YA KUMALIZA ELIMU MSINGI SINGIDA.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Mahembe Manispaa ya Singida wakifanya mitihani ya kumaliza elimu ya Msingi.

Wanafunzi elfu 21, 417 wa shule za Msingi 514 katika halmashauri saba za Mkoa wa Singida leo wameanza mitihani ya kumaliza elimu ya msingi inayofanyika nchini kote.

Wanafunzi hao mabao wavulana ni elfu 9,639 wasichana ni elfu 11,778 wamefanya mitihani ya masomo ya kiswahili, hisabati na sayansi kwa siku ya leo huku wakimalizia na masomo ya kiingereza na maarifa ya jamii.

Afisa Elimu Mkoa wa Singida Florian Kimolo amesema mitihani inafanyika kwa amani na utulkivu kutokana na kufanya maadalizi mapema kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na halmashauri zote za Mkoa wa Singida.

Kimolo ameongeza kuwa Mkoa ulitoa semina nelekezi kwa waalimu wasimamizi 2158 ambao wanasimamia mitihani katika shule 511 zenye wanafunzi wanaofanya mitihani hiyo ikiwa shule za serikali ni 504 na za binafsi 7.

Amesema kuwa wanafunzi wasioona wanaofanya mitihani ni 8 wavulana watano na wasichana watatu huku wenye uoni hafifu ni 49 wavulana wakiwa 23 na wasichana 26.

Akiongea baada ya kuanza kwa mitihani katika shule ya Msingi Mahembe iliyopo Manispaa ya Singida Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwana Patrick Masong amesema mitihani inafanyika kwa utulivu na watahiniwa wote wamehudhuria.

Masong amesema hakuna matatizo yoyote yaliyojitokeza tangu waanze mitihani na wana imani zoezi hilo litakamilika kwa usalama huku akisema ufaulu utakuwa mzuri kutoka na walimu kuwafundisha vizuri wanafunzi hao.


Mmoja kati ya Wanafunzi wa shule ya Msingi Mahembe Manispaa ya Singida akifanya mitihani ya kumaliza elimu ya Msingi.
 

Wanafunzi wa shule ya Msingi Mahembe Manispaa ya Singida wakifanya mitihani ya kumaliza elimu ya Msingi.

No comments:

Post a Comment