Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Mathew Mtigumwe (katikati) akiongozana na
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai (nyuma yake) na
ujumbe kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (mbele).
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Mathew Mtigumwe(Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Nguabiagai wakimsikiliza mmoja wa wajumbe wa kikundi cha wanawake wajasiriamali wakati akiwaelekeza namna ya kutengeneza tomato sauce na tomato paste.
Na Omary Mtamike, Mkalama
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe amesisitiza wakulima
kujiunga na vikundi vidogo na vikubwa
ili waweze kupatiwa Mikopo itakayowawezesha kuendeleza miradi yao kwa urahisi.
Mtigumwe ameyasema hayo alipofanya ziara mwisho wa wiki katika Kiwanda cha
kusindika zao la nyanya kinachotarajiwa kuanza kufanya kazi muda wowote kuanzia sasa ambapo kitasaidia
wakulima wanaolima zao hilo katika kata ya Gumanga na maeneo ya karibu kupata
sehemu ya kuuza mazao yao.
“Kupitia kiwanda hiki sasa mtaweza kuzalisha nyanya kwa
wingi kwa sababu mmeshapata sehemu ya kuuza badala ya awali ambapo mlikuwa
mkiuza kwa hasara au kuyaacha yakiharibika shambani”. Alisema Mtigumwe.
Akisisitiza kuhusu suala hilo la kujiunga na vikundi
Meneja wa Shirika la viwanda vidogo (SIDO) mkoani Singida , Shoma Kibende
alisema shirika hilo lina uwezo wa kukopesha kila mwanachama aliyepo kwenye
kikundi kiasi cha shilingi laki tano hivyo alishauri wanakijiji wa kata ya Gumanga
wajiunge kwenye vikundi ili iwe rahisi kwao kukopesheka.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida
alimmwagia sifa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai na safu
yote ya watendaji wake kwa kazi nzuri ya kutekeleza maagizo yote wanayopewa
huku ikiongoza katika kila kampeni za kitaifa zinazotangazwa ikiwemo ya maabara
pamoja na madawati.
“ Kwa kweli Mkalama mnastahili sifa sana kwa sababu kila
kampeni ya kitaifa mmekuwa mkiongoza kwa Mkoa wote wa Singida na nimeambiwa
hata hili la madawati mbali na kuongoza mpaka hivi sasa, mtalimaliza rasmi
tarehe 15 mwezi huu, hongereni sana”,
Alisema Mtigumwe.
Aliongeza juu ya hilo kwa kuwashauri wakurugenzi na
wenyeviti wa halmashauri za wilaya nyingine za mkoa huo kufika katika Wilaya ya
Mkalama na kujifunza ni namna gani
wanaweza kutekeleza maagizo kwa mafanikio.
Hili si ndoo ya Maji bali ni mtambo wa kutengeneza mvinyo kwa kutumia
nyanya kama ulivyowasilishwa na kikundi cha Wanawake wajasiriamali
katika Kata ya Gumanga.
No comments:
Post a Comment