Tuesday, June 21, 2016

WAZIRI KAIRUKI AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUFANYA VIKAO KAZI NA WATUMISHI WA MKOA WA SINGIDA














Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Mkoa wa Singida wakati wa kikao kazi na watendaji hao kilichofanyika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016.

















Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na Watumishi mbalimbali wa Mkoa wa Singida (hawapo pichani) alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016, Mkoani Singida, wanaofuata kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Mathew Mtigumwe, Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida,  Dkt. Angelina Lutambi na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Saidi Amanzi.

















Baadhi ya Watumishi wa umma Mkoani Singida wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016, Mkoani Singida.

















Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Dkt. John Mwombeki akifafanua jambo wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki na Watumishi wa Mkoa wa Singida ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe 16-23 Juni kila mwaka.


Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji akifafanua jambo wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki na Watumishi wa Mkoa wa Singida ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe 16-23 Juni kila mwaka.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (MB.) amewataka Watumishi wa Umma nchini waliopewa dhamana serikalini kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa ili kuepuka malalamiko yasiyo ya lazima kwa wanaowahudumia.
Waziri Kairuki ameyasema hayo wakati akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016 Mkoani Singida.
“Najua miongoni mwa watumishi wa umma wapo watumishi waliopewa dhamana lakini utoaji wao wahuduma unatiliwa shaka. Hawapendi kusikiliza matatizo ya wateja wa ndani yaani watumishi wenzao,” Mhe. Kairuki alisema.
Amewataka watumishi wenye tabia hizo kuacha mara moja na kuishi maisha ya kazi kama Mkataba wa Huduma kwa Mteja unavyowaongoza katika kutoa huduma kwa kiwango kwa wateja wote wa ndani na nje ya taasisi.
Aidha, Mhe. Kairuki amewataka Watendaji kutenga muda wa kukaa na watumishi wao ili kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.
“Uzoefu unaonyesha kuwa watumishi wanaposhirikishwa katika masuala yanayowagusa kama tulivyo hapa basi huduma kwa wananchi na wadau wengine zitaboreka na kazi kufanyika kwa ari na hivyo kuongeza tija na ufanisi kazini,” Waziri Kairuki aliongeza.
Katika hatua nyingine, Mhe. Kairuki alifanya ziara katika Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Singida na kuzungumza na watumishi wa chuo hicho ambapo aliwataka watumishi hao kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuwajibika ili kuleta matokeo bora kwa taifa.
“Tuwe wabunifu, tuangalie vipaumbele, tufundishe kozi ambazo hazifundishwi sehemu nyingine ili kuweza kupata soko zuri zaidi,” Waziri Kairuki amesisitiza.
Amewasisitiza watumishi hao kuwa na ushirikiano na vyuo mbalimbali hasa katika nyanja za utafiti, mafunzo na masuala mengine ya maendeleo ili kuboresha chuo hicho.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika kuanzia tarehe 16-23 Juni, kila mwaka, kwa mwaka 2016 yanafanyika kwa namna tofautia mbapo Viongozi na Watendaji wanakutana na wateja wao wa ndani na nje ya taasisi zao kwa lengo na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika kutekeleza hilo, Mhe. Kairuki amezindua maadhimisho hayo kwakufanya vikao kazi na watumishi wa mkoa wa Singida kutoka katika kada mbalimbali za utumishi wa umma.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika kwa mwaka 2016 ni “Uongozi wa Umma kwa ukuaji Jumuishi: kuelekea katika Afrika tunayoitaka.”
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akipokea Ripoti ya Utendaji wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Singida kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Chuo Cha Utumishiwa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo, wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Fedha na Utawala wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Bw. Rajabu Mirambo na Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Singida, Bw. Ramadhani Marijani
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na tawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kulia aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Singida mara baada ya kikao kazi na watumishi hao  ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe 16-23 Juni kila mwaka, kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo na kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.

No comments:

Post a Comment