Wednesday, June 22, 2016

MKUU WA MKOA AAGIZA WATENDAJI WANAOSABABISHA HOJA WACHUKULIWE HATUA.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng. Mathew Mtigumwe akizungumza katika baraza maalumu la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali. 
 
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakizungumza katika baraza maalumu la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.














Wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakiwa katika baraza maalumu la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng. Mathew Mtigumwe amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Supeet Roine Mseya kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria watendaji wote wanaosababisha hoja kwa uzembe au makusudi.

Mtigumwe ameasema hayo jana katika kikao cha baraza maalumu la madiwani la halmashauri ya Manyoni la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ambapo Halmashauri hiyo ina hoja 128 na ina hati yenye mashaka.

Ameongeza kuwa Mkurugenzi napaswa kuonyesha katika taarifa yake ni hatua gani ameichukua kulingana na ukubwa wa kosa kwa watendaji wake waliosababisha hoja.

Nao madiwani wa Halmashauri hiyo kwa pamoja wamesisitiza kuwa hatua za kinidhamu zinazochukuliwa na Mkurugenzi bado haziridhishi kulingana na makosa wanayotenda watumishi hao.

Madiwani hao wameongeza kwa kutroa mfano wa Mtendaji aliyepewa onyo kwa kuisababishia hasara halmashauri kwa kufanya manunuzi ya kujaza mitungi ya gesi kwa bei ya shilingi laki moja wakati bei ya soko ikiwa ni shilingi elfu 56 kuwa adhabu hiyo ni ndogo kulingana na kosa.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Supeet Roine Msuya amekubaliana na maoni ya baraza la madiwani na kuahidi kumchukulia hatua zaidi mtendaji huyo pamoja na watendaji wengine walioisababishia halmashauri kuwa na hoja na hivyo kupata hati yenye mashaka.

No comments:

Post a Comment