Wednesday, December 09, 2015

MKUU WA MKOA ATEMBELEA MIRADI YA EU KUWAKI


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Kone akikagua ujenzi wa jengo la kusindika mazao ya mbogamboga na matunda katika kijiji cha Gumanga Wilayani Mkalama.
 
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Kone akikagua shamba la mazao ya mbogamboga na matunda katika kijiji cha Gumanga Wilayani Mkalama.
 
 
Moja ya shamba la mbogamboga na matunda katika kijiji cha Gumanga Wilayani Mkalama, wakulima wa mazao hayo wako katika mradi wa EU KUWAKI.
 
 
Moja ya shamba la nyanya  katika kijiji cha Gumanga Wilayani Mkalama, wakulima wa nyanya hizo wako katika mradi wa EU KUWAKI.
 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Kone, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Christopher Ngubyagai na Meneja Mradi wa  EU KUWAKI Andrew Rwechungura wakiwa katika kikao cha wanakamati ya kusimamia mradi wa EU KUWAKI ili kutathmini maendeleo ya mradi huo unaolenga kuwakomboa wanawake kiuchumi kupitia kilimo cha mbogamboga na matunda Mkoani Singida.
 
 
Wanakamati ya kusimamia mradi wa EU KUWAKI wakitathmini maendeleo ya mradi huo unaolenga kuwakomboa wanawake kiuchumi kupitia kilimo cha mbogamboga na matunda Mkoani Singida.

No comments:

Post a Comment