Thursday, July 30, 2015

MKUU WA MKOA AZINDUA OFISI YA JUMUIYA YA WATUMIA MAJI MWITIJA MGORI, SINGIDA, 27 JULAI 2015.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V. Kone akimsalimia mshauri wa masuala ya kiufundi kutoka Shirika la Maendeleo la Serikali ya Sweden (SIDA) Jorge Maluenda, katikati ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida Aziza Mumba na nyuma ya Mkuu wa Mkoa ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Said Amanzi.
 
Katibu Mkuu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa(ALAT), Habraham Shamumoyo akitoa shukrani kwa shirika la SIDA kwa ufadhili wa ujenzi wa ofisi ya Jumuiya ya Watumia maji MWITIJA na kuiomba Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Mkuu wa Mkoa wa Singida kutatua changamoto ndogo ndogo ikiwemo uaptikanaji wa umeme wa REA.
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Hijjat Mwasumilwe akisoma taarifa fupi ya Mradi wa MWITIJA ulioko Mgori, Wilayani hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V. Kone na Mkuu wa Wilaya ya Singida Said Amanzi wakifurahia mara baada ya ufunguzi wa jingo la ofisi ya MWITIJA.
 
















 Baadhi ya wakazi wa Mgori Wilayani Singida wakiwa wanasukuma maji.

No comments:

Post a Comment