Friday, October 24, 2014

KIKAO KAZI CHAFANYIKA KWA NJIA YA KI-ELETRONIKI KWA MARA YA KWANZA KATIKA MIKOA YA SINGIDA, ARUSHA NA DODOMA.




Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akifuatilia mada wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi  na Mikoa ya Singida, Arusha,  Dodoma na Tume ya Mipango.

Mikoa ya Singida, Dodoma na Arusha imefanikiwa kufanya kikao kazi kwa njia ya kielektroniki kwa mara ya kwanza kati yao na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Hab Mkwizu.

Mkwizu amewataarifu washiriki wa kikao kazi hicho ambao ni Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Sehemu na Vitengo, kuwa kikao hicho ni mwanzo wa matumizi ya mikutano ya ki-elektroniki itakayokuwa inafanyika mara kwa mara.


Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan na Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Baraka Mhembano wakifuatilia kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya ki-elektroniki na Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan ameishukuru Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kuandaa kikao kazi kwa njia ya kielektroniki kwani hurahisisha garama za kuwaita watumishi wengi Dar es salaam.

Hassan ameongeza kuwa njia hiyo huweza kuwakutanisha watu wengi na kwa garama nafuu na kuhimiza kuwa njia hiyo iendelee kutumika hata katika vikao vingine.

Ameshauri kuwa njia hiyo itumike kutoa maafunzo mbalimbali kwa mfano mafunzo ya maadili ya utumishi wa umma hasa kwa watumishi waajiriwa wapya.

Akitimisha kikao kazi hicho ambacho Mikoa ya Kigoma na Manyara ilishindwa kushiriki, Mkwizu amesema watumishi wanapaswa kusimamia taratibu, sheria na kanuni za utumishi wa umma hasa katika kipindi cha uchaguzi.


























Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Sehemu na Vitengo na wakifuatilia kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya ki-elektroniki na Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma.


























Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan akifuatilia kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya ki-elektroniki na Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma.

No comments:

Post a Comment