Tuesday, May 27, 2014

UMISSETA 2014 MKOANI SINGIDA KUANZA RASMI LEO

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan akijiandaa kupiga mpira kama ishara ya ufunguzi wa Mashindano ya Umisseta Mkoa wa Singida 2014.

"Wanafunzi wenye uwezo wa kufanya vizuri katika michezo ndio hao hao wanaoonyesha uwezo wa kufanya vizuri katika masomo yao".

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan ametoa kauli hiyo leo asubuhi wakati akifungua rasmi mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (Umisseta) katika uwanja wa Sekondari ya Mwenge Mjini Singida.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan akipunga mkono kwa maandamano ya wanafunzi wanaoshiriki mashindano ya Umisseta Mkoa wa Singida 2014.

Liana amesema wanafunzi wanoshiriki mashindano ya Umisseta wanapaswa kufuata sheria na taratibu za michezo ili kufanikisha kuunda timu bora ya Mkoa itakayoleta ushindi kwa Mkoa na Kanda ya Kati.

Amesema Mkoa wa Singida unasifika kwa kufanya vizuri katika Michezo ya Riadha hivyo basi wanamichezo hao wahakikishe wanapata ushindi wa mchezo huo katika ngazi ya kanda na Taifa.

Liana amesema serikali imeruhusu michezo hiyo kwakuwa michezo ni ajira, upendo, ushirikiano, amani, na hujenga afya bora kwa wanamichezo hao.
Katibu Tawala Msaidizi Elimu, Fatuma Kilimia akitoa nasaha kwa wanafunzi wanaoshiriki mashindano ya Umisseta kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan kufungua mashindano hayo.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Elimu Fatuma Kilimia amewaasa wanafunzi hao kuonyesha nidhamu ya hali ya juu na kujituma kwani hizo ni silaha zitakazowasaidia kupata ushindi.

Kilimia amesema wanafunzi 555 kutoka halmashauri sita za Mkoa wa Singida wanashiriki mashindano hayo kwa muda wa siku nne ili kuunda timu ya Mkoa wa Singida itayaoshiriki mashindano hayo kwa ngazi ya Kanda ya kati.

Afisa Michezo Mkoa wa Singida Henry Kapella akifurahia maandamano ya wanafunzi wa Umisseta 2014 kutoka halmashauri sita za Mkoa wa Singida.

 
Wanafunzi wa Umisseta kutoka halmashauri ya Manyoni  Mkoa wa Singida wakipita mbele ya Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.


Wanafunzi wa Umisseta kutoka halmashauri ya Manyoni  Mkoa wa Singida wakipita mbele ya Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.

No comments:

Post a Comment