Wednesday, May 21, 2014

MAPOKEZI YA KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA MKOANI SINGIDA.


Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsalimia Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone mara baada ya kupokelewa katika kijiji cha Kazikazi, mpakani mwa Mkoa wa Singida na Tabora.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana jumatatu ameanza ziara ya siku nane Mkoani Singida kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama hicho akitokea Mkoani Tabora.

Kinana amepokelewa na viongozi mbalimbali Mkoani Singida katika kijiji cha Kazikazi kisha kupokea taarifa ya Mkoa na ya chama.


Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisoma taarifa ya Mkoa kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone.

Kinana alitembelea shule ya Sekondari ya Mgandu na kushuriki katika kupaua jengo la Maabara la Sekondari na kuweka kumbukumbu ya kupanda mti mbele ya maabara hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akishiriki kupaua jengo la Maabara la Sekondari ya  Mgandu.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipanda mti mbele ya jengo la Maabara ya Sekondari ya Magandu mara baada ya kushirki kupaua jengo hilo.

No comments:

Post a Comment