Monday, May 12, 2014

SEMINA KUHUSU SHUGHULI ZA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA) MKOANI SINGIDA
Washiriki wa semina kuhusu shughuli za Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Mkoani Singida wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Singida Mwl. Queen M. Mlozi, Kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi SSRA Ernest Urembo.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mwl. Queen Mlozi ametoa wito kwa Mamlaka ya Usimamizi  na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuishauri mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kutembelea wananchi katika maeneo mbalimbali ili kuwahamasisha na kujiunga na mifuko hiyo.

Mwl. Mlozi ametoa wito huo leo asubuhi wakati akifungua semina kwa watendaji Mkoani Singida  kuhusu shughuli za mamlaka hiyo na kuongeza kuwa mifuko ya jamii imekuwa ikijitangaza katika maonyesho.

Ameongeza kuwa lengo la mifuko ya jamii ni kiandaa jamii ifaidike na uwekezaji na uendeshaji mzuri wa Mifuko hiyo kabla na wakati wa uzeeni.


Mkuu wa Wilaya ya Singida Mwl. Queen M. Mlozi akifungua semina kuhusu SSRA, Kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi SSRA Ernest Urembo.

Mwl. Mlozi ametoa rai kwa Mamlaka hiyo kujituma katika kutoa taarifa kwa wananchi na wanachama kuhusu haki zao kwa mujibu wa sheria.

Pia amewataka watendaji kutoka halmashauri mbalimbali Mkoani Singida kutoa elimu kwa wafanyakazi kuhusu manufaa ya kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Mmoja wa washiriki ameitaka Mamlaka kuzisimamia mifuko ya jamii kwa ukaribu zaidi kwani mifuko hiyo imekuwa ikijitokeza kwa wingi kukusanya wateja na kuondoka pasipo kurudi kutoa elimu na taarifa kwa wanachama wao.

Baadhi ya washiriki wa Semina kuhusu Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Mkoani Singida.


Baadhi ya washiriki wa Semina kuhusu Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Mkoani Singida.

No comments:

Post a Comment