Thursday, March 20, 2014

UGENI KUTOKA BENKI YA DUNIA


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone amepokea ugeni kutoka Benki ya Dunia ambao unafanya tathmini ya manufaa ya ujenzi wa mradi wa barabara ya lami ya Singida-Shelui yenye urefu wa kilomita 109.
 
Akiongoza ugeni huo jana asubuhi, Afisa mawasiliano kutoka Benki ya Dunia Loy Nabeta amesema lengo ni kutathmini manufaa ya barabara hiyo iliyojengwa kwa ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania.

Nabeta amesema licha ya kuwatembelea wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara hiyo,  ugeni huo utazungumza na wasafirishaji ili kufahamu manufaa waliyoyapata kutokana na ujenzi wa barabara hiyo.

Kwa upande wake Dk Kone amesema barabara hiyo ina manufaa makubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa baadhi ya manufaa hayo ni pamoja na kuongezeka kwa viwanda vidogovidogo vya kusindika mazao, Ujenzi wa nyumba bora kutokana na upatikanaji wa vifaa kwa urahisi, ulinzi na usalama kuboreka zaidi kutokana na kufikika kwa uharaka zaidi katika maeneo mbalimbali.

Dk Kone amesema katika kuhakikisha barabara zinatunzwa, wakuu wa wilaya, maafisa Tarafa, watendaji wa kata na wananchi waishio pembezoni wana wajibu wa kuhakikisha barabara hizo zinatunzwa.



Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Dunia, Wa kwanza kushoto kwake ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida mhandisi Yustaki Kangole na anayefuatia ni Afisa Mawasiliano toka Benki ya Dunia Loy Nabeta.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone akisisita jambo wakati akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Dunia, Wa kwanza kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.

Waandishi wa habari wakifuatilia mazungumzo ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone na ugeni toka Benki ya Dunia.

No comments:

Post a Comment