Tuesday, March 18, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA TAIFA YA KUTUNDIKA MIZINGA YA NYUKI MKOANI SINGIDA

Kauli Mbiu ya mwaka huu ni: “Boresha Ufugaji Nyuki, Linda Ubora wa Mazao Yake”. 

Madhumuni ya siku hii ni kuendeleza Ufugaji Nyuki unaolenga kuongeza idadi ya wafuga nyuki, usimamizi bora wa makundi ya nyuki na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa kuzingatia ubora na teknolojia za kisasa. Aidha, siku hii inatumika kuhamasisha uhifadhi endelevu wa raslimali za misitu na nyuki.

Siku hii ni chachu ya kuwahamasisha wadau na wananchi kwa ujumla kushiriki kwa wingi katika ufugaji nyuki wa kisasa. Maadhimisho haya Mkoani Singida yamefanyika katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone ameadhimisha siku hii kwa kushiriki pamoja na wanakikundi cha "Nyuki ni Mtaji" katika kutundika mizinga ya nyuki.

Dk Kone amesema jamii inapaswa kulinda misitu kwani nyuki huzaliana eneo lenye misitu na maji, pia ameshawashauri wanakijiji kuweka utaratibu wa kupanda miti katika makazi yao na kutundika mizinga angalau miwili kwa kila kaya.

Akisoma risala ya kikundi, Katibu wa kikundi cha "Nyuki ni Mtaji" Bw Mathew Gunda amemshukuru Dk Kone kwa jitihada zake za kuwasaidia wafugaji nyuki na pia ameiomba Serikali ya Mkoa iwasaidie kukarabati bwawa lililopo katika msitu huo na mafunzo ya utaalamu zaidi wa ufugaji nyuki wa kisasa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone akisaidiwa kuubeba mzinga wa nyuki na Afisa Nyuki Wilaya ya Manyoni Chesco Lunyungu ili aweze kuutundika katika msitu wa kijiji cha Nkungi wilaya ya Mkalama. 
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan akisaidiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP Geofrey Kamwela kuubeba mzinga wa nyuki na kuutundika katika msitu wa kijiji cha Nkungi wilaya ya Mkalama.
Afisa wa Magereza Mkoa wa Singida SACP Agatha Komba akisaidiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP Geofrey Kamwela kupaka nta katika mzinga wa nyuki na kisha kuutundika katika msitu wa kijiji cha Nkungi wilaya ya Mkalama.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone akipokea risala ya kikundi cha ufugaji nyuki cha "Nyuki ni Mtaji" katika maadhimisho ya siku ya kitaifa ya kutundika mizinga Mkoani Singida yaliyofanyika katika msitu wa kijiji cha Nkungi wilaya ya Mkalama.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone akipokea Zawadi ya asali kutoka kwa kikundi cha ufugaji nyuki cha "Nyuki ni Mtaji" katika maadhimisho ya siku ya kitaifa ya kutundika mizinga Mkoani Singida yaliyofanyika katika msitu wa kijiji cha Nkungi wilaya ya Mkalama.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan akipokea Zawadi ya asali kutoka kwa kikundi cha ufugaji nyuki cha "Nyuki ni Mtaji" katika maadhimisho ya siku ya kitaifa ya kutundika mizinga Mkoani Singida yaliyofanyika katika msitu wa kijiji cha Nkungi wilaya ya Mkalama.
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida Bi Aziza  Mumba (wa kwanza kulia) akifuatilia kwa umakini maadhimisho ya siku ya kitaifa ya kutundika mizinga Mkoani Singida yaliyofanyika katika msitu wa kijiji cha Nkungi wilaya ya Mkalama.

No comments:

Post a Comment