Friday, March 28, 2014

MAHAKAMA YA TANZANIA KATIKA MAFUNZO YA KUTUNZA KUMBUKUMBU MKOANI SINGIDA, MACHI 26, 2014.

Watunza kumbukumbu 12 kutoka Mahakama ya Tanzania wamefanya ziara ya mafunzo juu ya utunzaji wa kumbukumbu katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.

Wakiongozwa na Afisa Tawala Mwandamizi Mahakama ya Tanzania Wanyenda Philip Kutta watunza kumbukumbu hao wamesema wamejifunza mambo mengi kutoka ofisi ya kumbukumbu ya Mkoa wa Singida.

Kutta amesema wameweza kujifunza kwa ufasaha kutokana na ushirikiano walioupata kutoka kwa watunza kumbukumbu wa Mkoa wa Singida wenye moyo wa kufundisha wenzao na wao wenyewe kujifunza kutoka kwa wenzao. 
Watunza kumbukumbu kutoka Mahakama ya Tanzania na watunza kumbukumbu wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida wakiwa katika picha ya pamoja  na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan (katikati).
Kwa upande wake mtunza kumbukumbu Mkaluzima Mashoka amesema amejifunza utendaji mzuri wa kazi na mpangilio mzuri wa nyaraka ambao ujuzi huo utamsaidia katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

Mashoka amesema ziara hiyo imewanufaisha watunza kumbukumbu ambapo wameweza kuona jinsi nwenzao wa mikoa na wizara mbalimbali hasa Mkoa wa Singida wanavyotunza kumbukumbu kwa ufasaha zaidi.
Mtunza kumbukumbu kutoka Mahakama ya Tanzania Mkaluzima Mashoka akifurahia jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.
Naye mtunza kumbukumbu kutoka Makama ya Ardhi Dora Mbise amesema amejifunza utaratibu mpya wa kupokea barua ambao ni bora zaidi ya ule waliokuwa wakiutumia hapo kabla.
 
Mbise amesema utaratibu mwingine waliojifunza ni wa kuwa na majalada mawili, jalada kuu na jalada la kufanyia kazi,utaratibu ambao amesema ni mzuri na unasaidia katika kutunza kumbukumbu za ofisi vizuri.
Mtunza kumbukumbu Dora Mbise(wa pili kulia) akiwa na watunza kumbukumbu wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Ella Rajila,  Ester Hadu na Agnes Temu.
Naye Mtunza kumbukumbu Salum M. Salum kutoka Mahakama Kuu ametoa rai kwa watunza kumbukumbu wenzake kufuata taratibu na kanuni za utunzaji kumbukumbu ambazo zina fanana nchi nzima.

Salum amesema mtunza kumbukumbu yeyote anapofuata kanuni na taratibu zitamuongoza vema na iwapo atakiuka taratibu na kanuni hizo atashindwa kutekeleza majukumu yake vizuri.

Mtunza kumbukumbu Salum M. Salum kutoka Mahakama Kuu masijala ya siri.
Mkoa wa Singida umeteuliwa kwa ajili ya mafunzo hayo kwa kuwa ni moja wapo kati ya Mikoa miwili na Wizara tatu ambazo zimefanya vizuri katika utunzaji wa kumbukumbu ambayo ni Mkoa wa Manyara, Wizara ya Mambo ya Ndani, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dodoma, Ofisi ya rais Utumishi wa Umma.

Kwa niaba ya watunza kumbukumbu hao kiongozi wa ziara hiyo  Afisa Tawala Mwandamizi Mahakama ya Tanzania Wanyenda Philip Kutta ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Singida kwa ukarimu wao na kuahidi kuendeleza yale waliyojifunza.
Watunza kumbukumbu kutoka Mahakama ya Tanzania wakipata chakula cha pamoja na watunza kumbukumbu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

No comments:

Post a Comment