Wednesday, June 07, 2023

Tupande miti ya vivuli na matunda katika miradi niliyoitembelea" RC Serukamba.

 

RC Serukamba amesema kila Mkuu wa Shule aone umuhimu wa kuendeleza zoezi la utunzaji wa mazingira kwa upandaji miti, nyasi na matunda katika maeneo ya shule ili wanafunzi wapate mahali pa kupumzikia na matunda kwa ajili ya kuboresha afya zao.

Maelekezo hayo ameyatoa leo  tarehe 06.06.2023 akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Ikungi katika Shule ya Msingi Matare iliyopo kata ya  Unyahati ambapo akimshukuru Mkuu wa Shule kwa usimamizi mzuri wa ujenzi huo pamoja na kujionea kilimo cha migomba kilichoshamiri eneo hilo.

Amesema kwa nyakati hizi kila mtu anatakiwa kupambana na changamoto ya utapia mlo kwa watoto hivyo kuwashauri walimu wakuu kuendelea kusimamia kilimo cha bustani, miti na matunda kwa faida ya wanafunzi.

Serikali imekua ikitoa fedha kiasi cha Tsh. 1000 kwa kila mtoto kupitia Halmashauri lengo likiwa ni kuboresha lishe na kuondoa udumavu kwa watoto sasa ni wakati muafaka kwa shule kuwa na nyongeza ya mboga za majani na matunda kwa watoto.



RC Serukamba amezielekeza Halmashauri zote Mkoani hapo kuhakikisha wanazipatia shule miti ya kupanda maeneo yanayowazunguka na walimu wakuu kusimamia bustani za mboga na matunda.

Hata hivyo RC ameendelea kukagua miradi mbalimbali Wilayani Ikungi kwa siku ya pili mfululizo ambapo leo amekagua Mradi wa maji Kata ya Unyahati Kijiji cha Matare ulio gharimu jumla ya Tsh. Milioni 386.8 ambapo inategemewa kuhudumia wakazi 5036.

Miradi mingine ni shule za msingi za Dung'unyi, Ikungi B, na Shule ya Msingi Matare na Hospitali ya Wilaya, Barabara  ya kutoka Ikungi kwenda Matongo yenye urefu wa km 1.5.



No comments:

Post a Comment