Friday, July 15, 2022

Mkandarasi asimimishwa kazi Manyoni

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa ameagiza Wakala wa barabara mjini na Vijijini TARURA Mkoa wa Singida  kuvunjwa kwa mkataba baina yao na Mkandarasi wa  Kampuni ya Bullem Investment limited  wanaojenga Barabara ya kutoka Kitongoji cha Majengo mpaka Hospitali ya wilaya kwa kushindwa kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo  Wilayani hapo baada ya kupata malalamiko ya wananchi wa maeneo hayo wakilalamikia kushindwa kukamilika kwa Barabara hiyo kwa kipindi kirefu na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo.

Aidha Waziri Mkuu akamuagiza Meneja TARURA Mkoa wa Singida kukagua na kumlipa Mkandarasi kulingana na asilimia zilizofikiwa katika Ujenzi wa Barabara hiyo na asilimia zilizobaki apatiwe Makandarasi mwingine atakayeweza kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Hata hivyo kutokana na kutokamilika kwa miradi mbalimbali Wilayani Manyoni ikiwemo Mpango wa wamachinga, Ujenzi wa masoko kutokutana na wananchi kusikiliza changamoto zao Waziri Mkuu akawahakikishi wananchi kwamba viongozi wote ambao walihusika katika kukwamisha miradi ya Serikali kutokamilika watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Malalamiko mengine ya   wananchi hao ilikuwa ni kutozwa fedha wakati wa kujifungua kina mama wajawazito ukosefu wa masoko huduma isiyoridhisha wa stand ya mabasi na madeni ya fidia ya ardhi ya wananchi.

Aidha Waziri Mkuu akawaahidi wananchi hao kushughulikia swala la madeni ya fidia za ardhi pamoja na changamoto ya Kodi huku akimtaka mkuu wa Mkoa kuhakikisha wanakuja kuwasikiliza wafanyabiashara wadogo maarufu Kama wamachinga ili kutatua changamoto zilizopo.

Matukio katika picha

Wananchi wa Wilaya ya Manyoni wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa wakati aliposimama kusikiliza kero za wananchi hao.

No comments:

Post a Comment